Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya
Tanzania CDF Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kukagua magari hayo ya
Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askari mbalimbali wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) hawaonekani (pichani) katika Kambi
ya Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam. Rais Dkt.
Magufuli ametoa maagizo kwa Kikosi hicho cha 95KJ kubeba Korosho zote zitakazo
nunuliwa na Serikali iwapo Wanunuzi wa Korosho hawatatii agizo la Serikali
ifikapo siku ya jumatatu saa kumi alaasiri.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo wakielekea kwenye viwanja vya Kambi ya 95KJ
kukagua magari ya Kikosi hicho ambayo yatatumika kubeba korosho katika mikoa ya
Kusini iwapo Wanunuzi wa Korosho hawatatii agizo la Serikali ifikapo siku ya
jumatatu saa kumi alaasiri.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Madereva wa Kikosi cha
Usafirishaji cha Jeshi 95KJ ambao wapo tayari kutekeleza maagizo ya Serikali
baada ya siku ya jumatatu saa 10 alaasiri iwapo Wanunuzi wa Korosho hawatanunua
korosho zilizopo katika mikoa ya kusini.
Askari mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) wakimsikiliza Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza katika Kikosi
cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya
Tanzania CDF Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kukagua magari hayo ya
Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment