Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kuhusu uamuzi wa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli wa kuahirisha Maadhimisho ya sherehe za Uhuru yaliyotarajiwa
kufanyika 9 Desemba, 2018, Kwenye ukumbi wa Mkuu wMkoa wa Lindi,
Novemba 20, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi
………………..
*Aagiza
fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9,
2018 na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shamrashamra hizo
ameelekeza zitumike kujenga hospitali mkoani Dodoma ambayo itaitwa Uhuru Hospitali.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumanne, Novemba 20, 2018) na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, Rais Dkt. Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi milioni 995.182
zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili
ya ujenzi wa hospitali mkoani Dodoma.
Waziri
Mkuu ametoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa mkoa wa
Lindi pamoja na wilaya zake katika kikao cha maandalizi ya shughuli za kuzima
Mwenge kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi wa Mkuu wa Mkoa wa
Lindi.
Amesema
hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo
na Chamwino kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam itakuwa
inawahudumia wakazi wa mkoa wa Dodoma
pamoja na wananchi wengine watakaokuwa mkoani humo.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya
waandae matukio watakayoyatekeleza katika maeneo yao yatakayoashiria maadhimisho ya siku ya
Uhuru. “Wanaweza kutumia siku hiyo kwa kufanya usafi maeneo ya wazi au kwenye
hospitali.”
Kufuatia
maagizo hayo, Waziri Mkuu amewataka wananchi katika maeneo yote nchini
wajiandae kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zitakazopangwa na wakuu wao wa
mikoa na wilaya kufanyika katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment