Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi
Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, kuhusu kuifanyia
matengenezo barabara ya Majimoto-Inyonga yenye urefu wa KM 130 kwa kiwango cha
changarawe, mkoani humo.
Kaimu
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin
Mwakabende, akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu
ukamilikaji wa Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe
mkoani humo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi
Joseph Nyamhanga, akitoka kukagua kingo za Daraja la Kavuu linalounganisha
Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limekamilika na limeanza kutumika kwa
magari yasiozidi tani 30.
Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa mita
85.344linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limegharimu kiasi
cha shilingi bilioni 2.718.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment