Naibu waziri Omary Mgumba
akiongea na wakulima wa kijiji cha ngulwe
Naibu Waziri Mgumba
akikagua maghara ya kuhifadhia mbolea mkoani Iringa
........................................
Naibu waziri wa Kilimo
Omari Mgumba Ametoa Onyo Kali Kwa Madalali Wanaowauzia Wakulima Wa Mazao Ya
Chakula Na Biashara Mbolea Kwa Bei Ya Shilingi Elfu sabini, 70,000 Badala Ya Kufuata Bei
Elekezi Ya Serikali Ya shilingi elfu sitini na nne na mia saba, 64,700 Kwa Mfuko Moja.
Akiwa Katika Ziara Mkoani
Iringa Ya Ukaguzi Wa
Upatikanaji Wa Mbolea Kwenye Maghara Ya Serikali Na
Wawekezaji Mkoani Hapa
Naibu Omar Amewataka
Madalali Hao Kuacha Mara Moja Tabia Hiyo Kwasababu Serikali Ya Awamu Ya Tano
Chini Ya Rais Magufuli Aina Utani katika Kuwasaidia Watu Masikini Na Wangonge.
Onyo ilo limetolewa Baada
Ya Wananchi Wa kijiji Cha Ngulwe Wilayani Kilolo Kutoa Malalamiko Yao Wakati Wa
Kikao Kilichowahusisha Wakulima Na Waziri Mgumba.
“Ndugu wananchi Nimeskia
Malalamiko Yenu Kuhusu Bei Ya Mbolea, Nataka Nitoe Rai Kwa Wauzaji Wa Mbolea
Nchi Nzima Atakauza Mbolea Kwa Bei Tofauti Na Ile Elekezi Iliyopangwa Na
Serikali Tutamchukulia Hatua Za Kisheria” Alisema Naibu Waziri Mgumba.
Aidha Naibu Waziri
Aliwatoa Wasiwasi Wakulima Wote Nchini Kuhusu Upatikaji Wa Mbolea Na Pemebejio
Katika Kipindi Ichi Kuelekea Msimu Wa Kilimo Serikali Imejizatiti Kikamilifu Na
Mbolea Ipo Ya Kutosha Na Inauzwa Kwa Bei Elekezi Iliyotolewa Na Serikali.
Wakulima Wengi Nchini
Wamekuwa Katika Changamoto Ya Upatikanaji Wa Mbolea Ambapo Hapo Awali Kulikuwa Na
Waangizaji Zaidi Ya mmoja Hali Iliyopelekea Usumbufu Kwa Wakulima Na Bei Kuwa
Kubwa
Jambo Lilifanya Ambalo
Serikali kuingilia Kati Kwa Kuweka Wakala Maalum Wa Kuagiza Mbolea Kutoka Njee
Ya Nchi Na Kutoa Bei Elekezi Kwa Wauzaji.
Msimu Wa Kilimo Unatarajia
Kuanza Hivi Karibu Kutegemea Unyeshaji Wa Mvua za Masika Nchini Ambapo Mikoa Ya
Nyanda Za juu Kusini Ndio Inategemewa Kwa Uzalishaji Wa Kiwango Kikubwa Cha
Mazao Ya Biashara Na Chakula
No comments:
Post a Comment