Posts

Showing posts from May, 2024

DED BAGAMOYO AFUNGUA MAFUNZO KUHUSU MABORESHO YA MITAALA YA ELIMU YA AWALI, MSINGI, SEKONDARI NA UALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI BAGAMOYO MKOANI PWANI.

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw Shauri Selenda tarehe 30 Mei 2024 amefungua mafunzo kuhusu maboresho ya mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo Mkoani Pwani. Mafunzo hayo, yamelenga kuwapitisha washiriki katika muundo wa Elimu, Maboresho Elimu Msingi na Sekondari pamoja na Ualimu. " Ndugu zangu nyinyi mliopo hapa ni asilimia ndogo sana ya washiriki wanaohitajika kupata mafunzo haya, hivyo nawaomba muwe makini kutumia muda Ili muweze kupata Yale yaliyotarajiwa kutoka kwa wawezeshaji wetu ". Alisema Bw Selenda. Mafunzo haya ya siku mbili  yanajumuisha Walimu Wakuu 78 toka Shule za Msingi za Serikali na binafsi Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Ofisi ya Raisi- TAMISEMI

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2024

Image
SOMA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI KWA MWAKA 2024. UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2024 CHAGUA MKOA ULIKOSOMA CHAGUA MKOA ULIKOSOMA ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA GEITA IRINGA KAGERA KATAVI KIGOMA KILIMANJARO LINDI MANYARA MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA NJOMBE PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SIMIYU SINGIDA SONGWE TABORA TANGA

MKOA WA KAGERA KUANZISHA MASHAMBA YA KAHAWA ZAIDI YA HEKTA 4,000

Image
  Na Alodia Dominick, Bukoba. Mkoa wa Kagera unatarajia kuanzisha mashamba ya pamoja ya kahawa zaidi ya hekta 4,000 lengo likiwa ni kuondoa umaskini kwa wananchi wa mkoa huo. Hayo yamebainika katika mkutano wa wadau wa kahawa uliofanyika Mei 29, mwaka huu katika ukumbi wa mkuu wa mkoa huo. Akifungua mkutano huo mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa, amesema kuwa, kuanzishwa kwa mashamba ya pamoja ya  kahawa ni agizo la Wizara ya kilimo ililolitoa hivi karibuni kwa bodi ya kahawa Tanzania (TCB) kuhakikisha inatoa matrekta na Wizara itatoa miche ya mibuni zaidi ya milioni 5. "Dhamira ya serikali ni kupanua kilimo cha kahawa, sote tunayo kumbukumbu kahawa ilivyokosa bei wakulima wengi walikata miche ya kahawa hivyo mashamba mengi yana miche michache ya kahawa na tunao uwezo wa kuzalisha mara mbili ya kahawa  tuliyo nayo katika mkoa wetu wa Kagera" "Tukifanya hivyo hata ile ya kutajwa tajwa eti sisi ni wa pili kutoka mwisho kwa umaskini itaisha tutakuwa tunashikilia namb...

MWENGE WA UHURU WAZINDUA KLABU YA WAPINGA RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA  GREAT MINDS SCHOOL 

Image
  NA HADIJA OMARY, LINDI Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2024 Godfrey mnzava amezindua klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za kulevya ya shule ya Great minds primary school iliyopo Halmashauri ya manispaa ya Lindi Mkoani Lindi . Uzinduzi huo ulioenda sambamba kwa Shule hiyo kukabidhiwa  cheti cha ufunguzi,  uzinduzi rasm wa klabu hiyo ulifanyika jana   katika viwanja vya shule ya msingi Mnazi Mmoja Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ambako mkesha wa mwenge huo wa uhuru ulifanyika. Akizungumza na wanafunzi, walimu , viongozi alioambapatana nao pamoja na wananchi waliojitokeza katika viwanja hivyo Mnzava  aliwataka wanafunzi na wana klabu hiyo kuendelea kujifunza vizuri maswala hayo ya Rushwa na mapambano dhidi ya Dawa za kulevya ili wawe mabalozi wazuri kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. Awali akisoma risala kwa kiongozi huyo,  Anjela Lukanga mwanafunzi wa shule ya Great minds, amesema klabu hiyo ina jumla ya wananchama 33 ambapo kati yao w...

TAWI LA UDSM KUJENGWA KAGERA.

Image
  Na Alodia Babara, Bukoba Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa ametaja manufaa manne yatakayopatikana baada ya kukamilika ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam ikiwemo kupanua mji, kukuza uchumi, kuongeza fursa kwa vijana wa Kagera na kuongeza urafiki. Tawi hilo la chuo kikuu litajengwa katika kijiji cha Itahwa kata ya Kalabagaine halmashauri ya Bukoba na eneo la chuo hicho ni hekali 315 ambazo zilitolewa na wananchi wa vijiji viwili vya Kangabusharo na Itahwa na hafla  ya kukabidhi eneo la ujenzi kwa mkandarasi imefanyika Mei 29,mwaka huu. Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa akiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo litakapojengwa tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam amewashukuru  wananchi kwa kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na kutoa manufaa manne yatakayopatikana baada ya kukamilika kwake. "Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutukumbuka wanakagera kutuletea fedha kw...

KLABU ZA WAPINGA RUSHWA MASHULENI ZINASAIDIA KUENDELEZA  MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Image
  Na Hadija Omary, Lindi. Imeelezwa kuwa Kuanzishwa kwa klabu za wapinga rushwa mashuleni ni chachu ya kuimarisha na kuhamasisha wanafunzi kupenda kushiriki kwenye vitendo vya kuzuia, kupinga na kupambana na rushwa katika jamii. Hayo yameelezwa na  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024,  Godfrey  Mnzava alipotembelea Klabu ya Wapinga Rushwa ya Shule ya Sekondari Hawa Mchopa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi. Kwa lengo la kuimarisha klabu hiyo. Mnzava  amesema kuwa kwa kuzingatia kauli mbiu ya KUZUIA RUSHWA NIJUKUMU LAKO NA LANGU, TUTIMIZE WAJIBU WETU,  jamii inapaswa kuendelea kutoa msisitizo na kuwekeza zaidi katika kuelimisha wanafunzi ambao ndio viongozi wa kesho ili waweze kujua madhara ya Rushwa kwa jamii. "Tuweke nguvu zaidi katika kuunda klabu za wapinga rushwa mashuleni na vyuoni ili kuwaandaa hawa viongozi wetu wa kesho kujua madhara ya rushwa na kuichukua rushwa ili tuweze kujenga taifa la watu wanaoichukia rushwa...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI.

Image
  Wizara ya Ujenzi imeanza utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa ubia (PPP)katika kutekeleza miradi ya miundombinu. Haya yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024 Amesema ni katika kuipunguzia Serikali gharama kubwa za utekelezaji wa miradi ya miundombinu hasa barabara na madaraja ambayo Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha. “Lengo la kutumia utaratibu huu ni kujenga miundombinu na kuitekeleza kwa wakati.” Aliitaja iradi inayotekelezwa kwa utaratibu huo kuwa ujenzi wa barabara ya Kibaha-Chalinze-Morogoro-Dodoma (Expressway) yenye urefu wa kilometa 423.8 kwa mfumo wa kulipia.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2024 AWAPA HEKO MTAMA KWA KUANZISHA KITUO CHA REDIO

Image
  Na HADIJA OMARY, LINDI kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameipongeza halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi kwa uibuaji wa mradi wa  kituo cha kurusha matangazo cha Redio Mtama. Mradi huo wa ujenzi wa studio za redio jamii Mtama FM(106.3) uliibuliwa mwaka 2023 chini ya ufadhili wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) uliopo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Akizungumza na wananchi mara baada ya mwenge wa uhuru kutembelea katika Redio hiyo iliyopo katika Mtaa wa majengo katika halmashauri hiyo  kiongozi huyo amesema mradi huo ni mzuri na kwamba utawezesha halmashauri kufikisha Taarifa kwa wananchi kwa uharaka. Hata hivyo Mnzava ameitaka  jamii kutumia kituo hicho ili kiweze kuleta tija kwao na kutoa wito kwa uongozi wa halmashauri kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa hatua zilizobaki ili kiweze kuanza kutumika kwa wakati. Aidha Mnzava ametumia fursa hiyo kueleza umuhimu wa vyombo vya habari na kauli mbiu ya Mwenge ...

UPOTOSHAJI WA VIVUKO KIGAMBONI UNA MASLAHI BINAFSI: WAZIRI BASHUNGWA

Image
  Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewatoa hofu Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wanaotumia usafiri wa vivuko eneo la Kigamboni -Magogoni juu ya taharuki kuhusu huduma inayotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) nakueleza kuwa imetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi. Ameyasema hayo leo Mei 28, 2024 wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha inaimarisha huduma ya usafiri wa vivuko nchini. "Niwatoe wasiwasi Wananchi wa Dar es salaam pamoja na kigamboni, taharuki ambayo imetengenezwa hakukuwa na sababu ya kutengenezwa. Lakini sisi tunaofahamu yapo maslahi binafsi nyuma ya utengenezaji wa hii taharuki" Amekaririwa Bashungwa Ameeleza kuwa sasa vivuko vingi vinaendelea na matengenezo, lakini pia Mkandarasi Songoro Marine anaendelea na ujenzi wa vivuko vipya katika karakana yake mkoani Mwanza kwa ajili yakupelekwa kwenye maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wananchi. Aidha, Bashung...

ZAIDI YA WANANCHI 6,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MTAMA

Image
  Na Hadija Omary, Lindi Zaidi ya  watu  6,000 wa vijiji vya Chiuta, Mikongi na maeneo ya jirani katika halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wameanza kunufaika na upatikanaji wa huduma ya uhakika ya maji safi na salama. Hiyo ni baada ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Mzava kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya maji Chiuta -Mikongi, Mei 27,2024. Mradi huo unaogharimu Kiasi  cha zaidi ya Milioni 452 umeboreshwa kwa lengo la kukidhi mahitaji halisi ya wananchi wa vijiji vya Chiuta na Mikongi ambapo  hapo awali  ulikuwa unatoa huduma ya maji chini ya asilimia 30 ya mahitaji halisi kwa jamii ya Kijiji cha Chiuta Pekee. Akitoa taarifa ya mradi mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Mhandisi wa mradi huo Olaph John  amesema mradi huo unatekelezwa na Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Masasi kwa kushirikiana na Shirika la World Vision kwa usimamizi wa Serikali kupitia wakala wa maji ...

BARABARA YA NYENGEDI-RONDO KUJENGEWA KWA KIWANGO CHA LAMI.

Image
  Na Hadija Omary, Lindi Hatua ya Serikali kupitia wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA) kuanza kujenga Mradi wa barabara ya Nyengedi-Mnara -Rondo yenye urefu wa km 1.15 kwa gharama ya Shilingi milioni 939,107,800.00 kwa kiwango cha lami kumeleta faraja  kwa wananchi wa vijiji hivyo. Ujenzi wa Barabara hiyo umewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mzava mei 27, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa halmashauri ya Mtama na hivyo kupunguza gharama za matengenezo ya kila mwaka. Kabla ya kuweka jiwe la msingi kiongozi huyo wa Mwenge wa uhuru Kitaifa,  ameeleza matumaini yake juu ya mradi huo kuwa utakamilika kwa wakati uliopangwa mwezi Oktoba Kama mkataba unavyoelekeza huku akiwahimiza Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) kusimamia vizuri ili wanachi wapate unafuu wa huduma ambazo zitategemea barabara hiyo. Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa...

LUGANGIRA KUANZISHA MABINT CUP KAGERA.

Image
  Mbunge viti maalum (CCM) mkoa wa Kagera Neema Lugangira akizumgumza na waandishi wa habari hawako pichani ......................... Na A lodia Babara,  Bukoba Mbunge viti maalum (CCM) mkoani Kagera Neema Lugangira ameanza maandalizi ya ligi ya mpira wa miguu  maarufu kama Mabintcup itakayowahusisha watoto wa kike na wanawake. Maandalizi ya ligi hiyo tayari yameanza kwa kuunda kamati tendaji ambayo wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Katibu wa chama cha soka mkoa wa Kagera Alhaji Amir, mkurugenzi wa Bukoba tour Wiliam Ruta, mwenyekiti wa chama cha soka wanawake mkoa wa Kagera Dkt Leonia Kaijage, mtu wa habari za mitandaoni na yeye mbunge Lugangira akiwa ni mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo itashirikiana na watu wengine.                     Neema Lugangira mbunge viti maalum mkoani Kagera jana akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba ambao wamejiunga pamoja kwa hiyari y...

MILIONI 866 KUJENGA BARABARA KM 1.2 KWA KIWANGO CHA LAMI LIWALE

Image
  NA  HADIJA OMARY  LINDI. Wananchi wa Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,  kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 866,659,200.40 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kilometa 1.2  kwa kiwango cha lami katika Halmashauri hiyo. Wametoa shukurani hizo mara baada ya mwenge wa uhuru kufika Wilayani humo na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo wa mradi wa barabara ambao unatajwa utarahisisha usafirishaji wa mazao. Hamisi Rashidi, Dereva Boda boda amesema kipindi cha masika Barabara hiyo ilikuwa ikijaa maji mara kwa mara hali iliyopelekea kutopitika kwa urahisi kipindi hicho cha masika hivyo ujenzi wa barabara hiyo unaenda kumaliza kero hiyo. Kwa mujibu wa Meneja wa wakala wa Barabara za mijini na vijijini TARURA Wilayani Liwale, Mhandisi. Living Stone Shija, amesema mradi huo wa barabara ya Murua-Mkurunguche- Ngojwike - Mandepe petrol station  unatekelezwa na mkandarasi M/...

WAKAZI WA MASAKI KISARAWE  WALILIA BARABARA

Image
Na Omary Mngindo, Kisarawe WAKAZI wa Vijiji vinavyounda Kata ya Masaki Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali kuandaa utaratibu wa Daladala nyingine zipitie barabara ya Kisanga kutokea Masaki. Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi kijijini Masaki wakazi Fatuma Swaiba, Juma Idd na Ramadhani Seif walisema kuwa kwa sasa usafiri unaotokea Chanika bodaboda nauli ni shilingi elfu tano. "Nauli yake kutoka Chanika mpaka kuanzia Kijiji cha Kisanga ni shilingi elfu 5,000 na kuendelea kutokana na umbali, lakini kuna umbali wa dakika 30 lakini upande wa barabara iko vizuri ukiachilia baadhi ya changamoto za maeneo machache," alisema Fatuma. Aliongeza kuwa kwa kutumia mabasi yanayotokea stendi ya mabasi ya Pugu kuelekea Kisarawe mjini na vijiji mbalimbali wanatozwa shilingi elfu 4,000,  hivyo wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupatikana kwa usafiri. "Kuna abiria wengine wanatokea maeneo ya Mkuranga na vitongoji vyake ambao kwanza wanafika pale Chanika, k...

SERIKALI KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MVUA-MAJALIWA

Image
  SERIKALI KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MVUA-MAJALIWA Asisitiza mpango wa Serikali wa kukuza sekta ya kilimo WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imejipanga kuendelea kurejesha miundombinu yote ya barabara zilizoathiriwa na mvua zilizonyesha nchini. Amesema hayo leo (Jumamosi Mei 25, 2024) alipokagua daraja lililopo katika kijiji cha Nambilanje ambalo limeharibika kutokana na mafuriko. Daraja hilo linaunganisha Wilaya za Liwale na Ruangwa. “Kwa wakati huu ambao barabara nyingi zimekatika na kuharibiwa na mvua, Sio mkoa wa Lindi pekee, eneo hili TANROADS wameshafika, wameangalia hii hali na Waziri wa Ujenzi ameshatoa taarifa kwamba wanaendelea na uhakiki” Amesema kuwa Serikali inasubiri taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu kuisha kwa mvua ili itoe fedha na kutangaza zabuni za ujenzi za ukarabati na matengenezo ya maeneo yote yaliyoathiriwa. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa w...

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AKOSHWA NA MRADI WA KITEGA UCHUMI WILAYA YA LIWALE 

Image
  KIONGOZI wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mzava  ameonyesha kuridhishwa na mradi wa  ujenzi wa vibanda 34 vya biashara katika eneo la stendi kuu ya mabasi Halmashauri ya wilaya ya Liwale  wenye Thamani ya shilingi milioni 137, 754, 450.00 Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuona utekelezaji wa mradi Mzava ameipongeza halmashauri hiyo kwa maono makubwa ya kuongeza chanzo kipya cha mapato  kitakachowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo  Hata hivyo Mzava ametoa siku tatu kwa halmashauri hiyo kuandaa mikataba mipya watakayoingia na wafanyabiashara wanaotumia vibanda hivyo " pamoja na kuwapongeza kwa kubuni chanzo cha mapato lakimi niwaagize halmashauri kuandaa mikataba mipya mutakayowapa wafanyabiashara hawa ambao wapo kwenye vibanda hivi ndani ya siku tatu kuanzia leo mei 25 hadi 29 mwenge wa uhuru uwe umeshapata taarifa ya utekelezaji wake" alisisitiza Mzava Kwa upande wake kaimu afisa Mipango wa halmashauri hiyo Ham...