MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Abdul Sharifu akimkabidhi jezi kwa mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kiromo Hosea Maganga
................................................
Na Omary
Mngindo, Kiromo Bagamoyo
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Abdul Sharifu
amekabidhi jezi kwa mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kiromo Hosea Maganga zitumike
kwa michezo mbalimbali.
Sharifu
amekabidhi jezi hizo kufuatia ombi kutoka kwa Tarki Mokiwa mwanafunzi wa shule
hiyo, wakati wa msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani, Farida
Mgomi, alipotembelea shuleni hapo, ambapo wanafunzi walielezea changamoto ya
vifaa.
Sharifu alisema
kuwa baada ya kupokelewa kwa changamoto hizo, yeye aliahidi jezi, Mwanaisha
Kikwete mipira wakati Mgomi akiahidi mipira, na kwamba yeye aliwasiliana na
mmoja wa marafiki zake wamempatia jezi hizo, na kwamba ameambiwa na Maganga
kuwa Kikwete ameshakabidhi mipira.
"Kwanza
niwapongeze kwa kuwa majasiri wa kuelezea changamoto zinazowakabili, msafara wa
Mwenyekiti ulipofika shuleni kwenu mlizungumza mambo mengi ikiwe vifaa vya
michezo, leo nawakabidhi," alisema Sharifu.
Aliongeza
kuwa kupatikana kwa jezi hizo na mipira iliyowasilishwa na Mwanaisha Kikwete
itaongeza hali ya michezo shuleni hapo, huku alisema kwamba baada ya kumalizika
kwa mitihani ya Kidato cha nne ataandaa michezo kati ya wahitinu na wanaobaki,
ataandaa zawadi.
"Jiandaeni
vizuri, baada ya kumalizika kwa mitihani nitaandaa michezo maalumu kati ya
wanaomaliza Kidato cha nne, na nyie mliobaki kwa maana ya kuanzia Kidato cha
kwanza mpaka cha tatu, nitaandaa zawadi nzuri," alisema Sharifu.
Akipokea
zawadi hizi, mwalimu Maganga alimahukuru Mwenyekiti huyo kwa kukabidhi ahadi
yake mapema, huku akiwataka wanafunzi kutumia vizuri jezi hizi, sanjali na
kujiimarisha kimasomo.
"Tunaimani
kubwa na Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dkt. John Magufuli, tunaona
dhamira yake, pia viongozi wa chama na Jumia zake mnatekeleza mnayoyaahidi,
mlikuja mwishoni mwa wiki, ndani ya siku tatu tumeona mlivyoviahidi,"
alisema Mwalimu Maganga.
Nae Mokiwa
kwaniaba ya wanafunzi wenzake wamemhaidi Sharifu kwamba watazitumia vizuri jezi
hizi, sanjali na kupatikana alama A kwenye mitihani yao yote wakati wakiwa
shuleni hapo.
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Abdul Sharifu akishusha jezi kwenye gari kwaajilia ya kuzigawa.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Abdul Sharifu akimkabidhi jezi kwa mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kiromo Hosea Maganga
No comments:
Post a Comment