Posts

Showing posts from June, 2016

RAIS, DKT JOHN MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WATATU.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akizungumza na wakuu wa mikoa aliowaapisha leo na wakuu wa wilaya, ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu aliowateua Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016. Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es salaam ni Dkt. Binilith Satano Mahenge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Charles Ogesa Mlingwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara na Bi. Zainab Rajab Telack ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa Mikoa imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wa wilaya wateule ambao waliteuliwa na Rais Magufuli Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016. Aidha, miongoni mwa wakuu wa wilaya 139 walioteuliwa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika wi...

TASUBA, YAPATA MKURUGENZI MPYA.

Image
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imepata mkurugenzi mtendaji mpya atakae ongoza chuo hicho kikongwe katika fani ya sanaa na utamaduni hapa nchini. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari leo, juni 28, 2016, ilisema kuwa, waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape mnauye, amemteua   Dkt. Herbert   F. Makoye, kuwa Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Uteuzi huo umefanywa chini ya kifungu namba   9. (1) cha sheria ya wakala wa serikali,   (Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa mamlaka waziri, ya kufanya uteuzi huo. Dkt. Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa uma. Dkt. Makoye ana shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka chuo kikuu cha Ghana na shahada ya Umahiri- (M. A. in Theatre Arts) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri mwandamizi wa Chuo...

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA ELIMU.

Image
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja za Wabunge mapema leo June 27, 2016 Bungeni  Mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja kuhusu muswaada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali  wa mwaka 2016. Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria ya Elimu kifungu kinachoeleza kuwa mtu anayempatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuwa adhabu yake ni faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo kisichozidi  miaka mitatu. “Muswada unapendekeza kuwa kifungu hicho kifutwe na badala yake kitungwe kifungu kipya cha 60A ili kuweka masharti yanayojitosheleza kuhusu zuio la kuoa au kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, kinapendekeza adhabu yake iwe kifungo cha miaka 30 gerezani,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju. Vile vile mtu atakayebainika kusaidia, kushawishi au kuacha mwanafunzi wa shule ya msingi a...

MECHI YA TP MAZEMBE NA YANGA WASHIBIKI WOTE KUINGIA BURE UWANJANI.

Image

MAJID HEMED MWANGA, ABAKI BAGAMOYO.

Image
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga. Kufuatia uteuzi mpya alioufanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Maguful, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, ameendelea kubaki wilayani Bagamoyo. Katika uteuzi huo wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani ni hawa wafuatao 1.       Bagamoyo        -           Alhaji Majid Hemed Mwanga 2.       Mkuranga       -           Filberto H. Sanga 3.       Rufiji           -           Juma Abdallah Njwayo 4.       Mafia            -           Sh...