Posts

Showing posts from 2024

WANAFUNZI KIDOGOZERO WAISHUKURU LION.

Image
  Na Omary Mngindo, Kidogozero. WANAFUNZI wanaioishi katika mazingira hatarishi wakilelewa kwenye kituo cha Faraja, Kijiji cha Kidogozero Kata ya Vigwaza Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameishukuru Lion Club (Host) ya jijini Dar esa Salaam kwa kuwapatia misaada. Shukrani hizo zimetolewa na wanafunzi Enjo Frank na Faraji Ramadhani baada ya kupokea vifaa vya shule na vyakula vyenye shilingi milioni 1.6, vikikabidhiwa na Rais Mahmood Rajvan, Mountazir Barwani na viongozi wenzao walipofika kijijini hapo kuwafariji watoto hao 41. "Namshukuru Mwenyeezimungu kwani sikutegemea kupata msaada kama huu, utakaonisaidia katika masomo yangu wakati shule ikifunguliwa, mungu awasaidie na awaongezee pale mlipopunguza," alisema Enjo. Nae Ramadhani alieleza kwamba kwa msaada huo wa begi, madaftari  pamoja na peni vimempatia chachu ya kuendelea na masomo, huku akiahidi kufanya vizuri zaidi katika elimu yake ya Sekondari. Kwa upande wao wazazi Mohamed Ally aliishukuru Lion huku akiwahi...

WAZIRI KIKWETE AHUDHURIA MASHINDANO YA QUR ANI KWA WENYE ULEMAVU.

Image
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Ridhiwani Kikwete  ameshiriki mashindano ya Usomaji wa Quraan Takatifu kwa Wenye Ulemavu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Riziki Lulida yaliyofanyika jijini Dodoma. Katika mashindano hayo ambayo yalikutanisha Wenye Ulemavu kutoka makundi mbalimbali, Waziri Kikwete alitoa  salamu za serikali na kuwakumbusha kazi nzuri anayoifanya Mh. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri Ya Muungano ya Tanzania ikiwemo Mkakati wa kusimamia Haki na Ustawi wa Wenye Ualbino, Sera ya Usimamizi wa Teknolojia saidizi na mapitizo ya sera mbalimbali zinazosimamia maslahi ya Wenye Ulemavu ikiwemo sera ambazo haziendani na mazingira ya sasa.  Aidha alisema Wizara kwa upande wao walieleza walipofikia katika kila maelekezo ya Mh. Rais, Ilani ya uchaguzi na miongozo mingi imetolewa.  Wameendelea kumpongeza Muandaaji wa mashindano hayo Bi. Riziki Lulida, na taasisi yake na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWAT...

WATU 7 WAFARIKI AJALI YA GARI KARAGWE.

Image
  Na Alodia Dominick,  Karagwe. Watu saba wamepoteza maisha huku wengine tisa wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ya haice, kosta pamoja na Lori aina ya scania katika kizuizi cha barabarani kilichopo kijiji cha Kihanga kata ya Kihanga wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva. Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea Desemba 03, 2024 saa 5:00 asubuhi  na kuhusisha lori aina ya scania yenye namba T621 AJQ lenye Tela namba T472 EAQ likiwa linatokea Kayanga wilaya ya Karagwe kwenda Kyaka lilipofika Kihanga katika kizuizi cha barabarani yalikuwepo magari mawili. Ameongeza kuwa, moja lilikuwa kosta namba T367 ECP pamoja na toyota  haice yenye namba za usajili T973 DGD yakiwa yamesimama yanaendelea kukaguliwa na maafisa uhamiaji mita kama kumi kutoka kwenye kizuizi ndipo Scania iliyagonga kutokea nyuma na kusababisha ajali hiyo. "Gari hilo limetokea ...

VIONGOZI WATEULE WA VITONGOJI NA VIJIJI WAAPA BAGAMOYO.

Image
  Viongozi wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Wajumbe wao walioshinda katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024. Leo tarehe 29 Novemba 2024 wameapishwa rasmi kushika nyadhifa zao katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.  Akifungua kikao cha kuwaapisha Viongozi hao, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bagamoyo Bw Shauri Selenda aliwakaribisha na kuwashukuru kwa kuchaguliwa  na kuaminiwa na wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 27 mwezi huu . "Nichukue nafasi kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba ya Halmashsuri kwa kuteuliwa kuwa viongozi wa Serikali za Mitaa,  "Mchakato haukuwa rahisi lakini mmefanikiwa niwapongeze". Alisema Bw Shauri Selenda.  Katika Uchaguzi huo ulifanyika tarehe 27 Novembe, 2024 vyama mbalimbali vya kisiasa vilishiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwenye vitongoji vyote   167 vya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.       Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Shaibu Ndem...

CCM YASHINDA KWA ASILIMIA 98.82 LINDI

Image
  NA HADIJA OMARY, LINDI. Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi Mkoani Humo bwana Juma Mnwele Leo tarehe 29 November 2024 ametangaza matokeo ya Jumla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji Katika Manispaa hiyo uliofanyika November 27 mwaka huu 2024 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake msimamizi huyo wa uchaguzi Manispaa ya Lindi amesema Kati ya nafasi za uongozi 1954 zilizoshindaniwa na Vyama vya siasa chama cha mapinduzi kimeshinda nafasi 1931 sawa na asilimia 98.82, chama cha ACT wazalendo wameshinda nafasi 21 sawa na asilimia 1.07 Alitaja chama chama kingine ni chadema ambacho kilishinda nafasi 2 sawa na asilimia 0.1 kikifuatiwa na chama cha wananchi cuf ambacho kimeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.05 huku chama cha CHAUMA, NCCR MAGEUZI na TLP vikikosa ushindi kabisa

RAIS SAMIA KUSHIRIKIANA NA THE ISLAMIC FOUNDATION KUANZISHA CHUO CHA UALIMU NA MAADILI.

Image
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameridhia kushirikiana na Taasisi ya The Islamic Foundation kuanzisha Chuo cha Ualimu na Maadili katika eneo la Kitungwa wilayani Morogoro. Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 25 Novemba 2024 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Msikiti wa Al Ghaith uliopo maeneo ya Kilakala Flats/old Dar es Salaam Road mjini Morogoro unaomilikiwa na Taasisi ya The Islamic Foundation Chini ya Mwenyekiti wake Aref Nahdi Aidha, Rais Dkt. Samia amesema katika kipindi hiki dunia imekumbwa na mmomonyoko wa maadili kuna haja kubwa ya kuongeza ujenzi wa Madrasa ili ziwe vituo vya kuwalea watoto kiimani na maadili. Aliwahimiza wazazi kusimamia malezi bora ya watoto ili jamii iwe na kizazi chenye hofu ya Mungu, na maadili mema. Akizungumzia mmomonyoko wa maadili, Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation, Aref Nahdi, amesema jamii ya sasa imecha ushirikiano katika malezi jamno linalopelekea watoto kupoteza heshima katika ...

HEART TO HEART YASAIDIA MRADI WA MAJI ZAHANATI YA NAMUPA

Image
  NA HADIJA OMARY,   LINDI. Hatua ya Taasisi ya heart to heart Foundation kwa ufadhili wa KOICA kuchimba kisima cha maji Katika Zahanati ya namupa iliyopo Katika Kata ya nyangao halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi  inaelezwa kuwa ni msaada kwa wanawake wajawazito wanaokwenda kujifungua Katika Zahanati hiyo kutobeba maji kutoka majumbani kwao Kwa mujibu wa taarifa ya Mganga Mfawidi wa Zahanati hiyo Dr. Paul Dominic alisema mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi victoria Mwanziva Jana November 15, 2024 wakati wa makabidhiano ya kisima hicho ni kwamba kutokana na  tatizo hilo la  ukosefu wa maji  Katika Zahanati hiyo inawalazimu kina mama wanaofika kwa ajili ya kujifungua  kubeba maji kutoka majumbani  " Katika kipindi ambacho kina mama walikuwa wanakuja kupatiwa huduma ya kujifungua Katika Zahanati yetu  walikuwa wanalazimika kubeba maji kutoka majumbani kwao na wengine wanabeba kutoka mtoni kwa ajili ya kuweza kusaidia kukabiliana na upungufu ...

GHOROFA LAPOROMOKA KARIAKOO

Image
  Jengo la ghorofa Kariakoo mtaa wa Kongo na Mchikichi Jijini Dar es aalaam limeporomoka leo asubui Novemba 16, 2024. huku watu kadhaa wakiwa chini ya kifusi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Charamila amefika eneo la tukio na kuwataka walio hai ndani ya jengo hilo wawe watulivu ili kuona namna ya kuwaokoa  Vikosi vya jeshi la ukoaji na zimamoto tayati vimewasili eneo la tukio, Vikosi vya jeshi la polisi vimefika eneo la tukio  Juhudi za kuokoa watu zinaendelea kwa kushirikiana vikosi vya jeshi la uokoaji na zimamoto, jeshi la polisi na wananchi wote waliopo eneo la tukio wakitoa ushirikiano

MUFTI NA SHEIK MKUU WA TANZANIA APONGEZA MRADI WA KUTAFSIRI QUR’AN TUKUFU NENO-KWA-NENO KWA LUGHA YA KISWAHILI

Image
  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally, amempongeza Dkt. Shehnaz Shaikh kwa kazi yake ya kujitolea katika kuandaa tafsiri ya Qur’an neno-kwa-neno kwa lugha ya Kiswahili.   Katika mkutano uliofanyika leo ofisini kwake Kinondoni, Dar es Salaam, mara baada ya swala ya Ijumaa, Dkt. Abubakary aliutambua mradi huo kama rasilimali nzuri kwa Waislamu wanaozungumza Kiswahili, na kwamba utawasaidia kuelewa Qur’an kwa undani wa kipekee.   Dkt. Shaikh, mzaliwa wa Gujarat, India, na kwa sasa akiishi Dallas, Marekani, aliandamana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu, Bi Shamim Khan, na Alhaj Albert Marwa, ambaye aliratibu ziara yake.    Dkt. Abubakary alitoa shukrani zake kwa kujitolea kwa Dkt. Shaikh, akibainisha kwamba ingawa wengi wanaweza kuelewa maana pana ya Qur’an, ni wachache wanaoweza kuifahamu kwa kina neno kwa neno.    Uelewa huu, alieleza, huleta muunganiko wa kiroho na uwazi zaidi wa mafundisho ya Qur’an, jambo a...

MATOKEO DARASA LA SABA 2024.

Image
  NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2024 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU SONGWE

DAKTARI KIZIMBANI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 12 BUKOBA.

Image
  Na Alodia Dominick, Bukoba Daktari wa viungo Haruna Ayubu maarufu kama Rubai (63) mkazi wa kata ya Rwamishenyi manispaa ya  Bukoba amepandishwa kizimbani kwa shitaka la ubakaji wa mtoto wa miaka 12. Rubai amefikishwa katika mahakama ya wilaya Bukoba Oktoba 23 mwaka huu na kusomewa kesi ya jinai namba 30251/2024. Upande wa mashtaka unaongozwa na mawakili wawili ambao ni Matilda Assey pamoja na Alice Mutungi. Akisoma maelezo ya awali wakili upande wa mashtaka amesema kuwa, kati ya Desemba 2023 na Oktoba 19, mwaka huu  mshitakiwa amekuwa akimuingiza mhanga katika moja ya chumba katika ofisi yake iliyopo mtaa wa Pwani, kata ya Miembeni manispaa ya Bukoba. Assey ameeleza kuwa, alipoingia katika chumba hicho alimvua mhanga nguo zake za ndani kisha na mshitakiwa kuvua nguo zake na kuchukua uume wake na kuuingiza kwenye uke wa mhanga baada ya mshitakiwa kumwingilia au kumbaka mhanga amekuwa akimpatia sh. 10,000 au 5,000 kwa ajili ya kuwapelekea wazazi wake. Aidha amesema, Oktob...

TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO KUZINDULIWA TAREHE 23 OKTOBA 2024

Image
  Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Tamasha la sanaa Bagamoyo, leo tarehe 22 Oktoba 2024. katika ukumbi wa TaSUBa mjini Bagamoyo. ................................. Na Athumani Shomari Mkwama. Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linatarajiwa kufunguliwa rasmi Tarehe 23 Oktoba 2024 katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa TaSUBa mjini Bagamoyo, Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wamejipanga kupokea wageni na kuwaburudisha kutokana na burudani za sanaa na utamaduni zitakazowasilishwa kwenye Tamasha hilo. Amesema TaSUBa imekuwa ikifanya tamasha kama hilo kila mwaka na kwamba kila mwaka linakuwa bora zaidi kuliko mwaka uliopita na mwaka huu pia litakuwa bora zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita. Am...

MTAALAMU BINGWA WA NYONGA NA MAGOTI KUTOKA UINGEREZA AWASILI DAR.

Image
Atashirikiana na wataalamu wa Mloganzila Na Mwandishi Wetu MTAALAMU bingwa wa upasuaji wa nyonga na magoti  kutoka hospitali ya Queen Elizabeth ya Uingereza Profesa Mamoun AbdelGadir, amewasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya kambi ya matibabu ya siku tano kwa watanzania. Daktari huyo kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani atafanya upasuaji huo kwenye kambi itakayofanyika katika hospitali ya Muhimbili Mloganzila  kuanzia Jumatatu 21,Oktoba 2024. Aliwasili leo  katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo alipokelewa na wafanyakazi wa Global Medicare ambao wameratibu kambi hiyo kwa kushirikiana na Muhimbili Mloganzila.  Akizungumza kwenye mapokezi hayo, Meneja Mkuu wa Global Medicare, Daniel Lazaro,  alisema wamefurahi kuona amefika salama nchini Tanzania na kwamba ujio wake utakuwa wa manufaa makubwa kwa watanzania wenye matatizo ya nyonga na magoti. “Tumefurahi kuona umefika salama na tunatarajia watanzania wengi watanufaika na ujio wako kwenye...

TRA KAGERA YAWAPA ELIMU YA KODI WAANDISHI WA HABARI.

Image
  Afisa uhusiano mkuu kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga, akizungumza katika mafunzo hayo. .............................................. Na Alodia Dominick, Bukoba Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) nchini imeendelea kusisitiza wananchi wanaponunua bidhaa yoyote kudai risit na wanapouza kutoa risit kwa kufanya hivyo pande zote zitakuwa zimechangia ulipaji kodi inayosaidia katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini. Afisa uhusiano mkuu kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga ameyasema hayo Oktoba 19,2024 wakati akizumgumza na waandishi wa habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka hiyo. Kamoga amesema, waandishi wa habari ni sehemu ya kuchochea maendeleo ya nchi yao na wanao wajibu wa kuelimisha jamii juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulipaji kodi kwani asilimia 70 ya mapato ya serikali inatokana na kodi huku asilimia inayosalia ikitokana na wahisani mbalimbali. "Unaponunua bidhaa ukadai risit unatimiza wajibu wako, risit ...

HOSPITALI YA SHIFAA YAZINDUA KITUO CHA TIBA NA UTAFITI WA SARATANI DAR

Image
  Picha mbalimbali wakati Waziri wa Afya,  Jenista Mhagama alipozindua kituo cha tiba na utafiti wa saratani katika hospitali ya Shifaa iliyoko Kinondoni barabara ya Msese jijini Dar es Salaam Ijumaaa Tarehe 11 Oktoba 2024. ....................................... Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Afya, Jenista Mhagama amezindua Kituo cha Tiba na Utafiti wa Saratani cha Shifaa na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuongeza bajeti ya dawa za saratani kila mwaka kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani. Waziri Mhagama aliyasema hayo Ijumaa jioni jijini Dar es Salaam wakati akizindua kituo hicho kilichopo kwenye hospitali ya Shifaa barabara ya Msese Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alisema wakati idadi ya wagonjwa ikiongezeka wagonjwa wengi wanaougua ugonjwa huo hawana uwezo wa kugharamia matibabu hivyo wanahitaji kusaidiwa. Alisema kwa mwaka huu wa fedha pekee serikali imetenga shilingi bilioni 10 kwaajili ya kununua dawa za saratani na kwamba kila bajeti mpya kiasi hicho kitaku...