Haji Jumaa mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Pwani akisisitiza jambo kwa wananchi wa
makulunge.
..................................................
Na Shushu
Joel, Bagamoyo.
WANANCHI wa
kata ya makulunge wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wamempokea mjumbe wa
halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa shangwe kubwa na matumaini wakiwa
na maana watendaji wote wa CCM ni watetezi wa watu wanyonge na wanaendana
katika utendaji wake.
Kilichopelekea
wananchi wa kata hiyo kumpokea MNEC huyo na wajumbe wake kwa shangwe
kubwa ni imani ya kuwa chanagamoto zao zilizokuwa zikiwabali kumalizika mara
moja.
Wakizungumza
katika mkutano wa hadhara kuhusu changamoto zao, wananchi hao walimwambia
MNEC huyo kuwa wamekuwa wakinyanyasika sana kuhusu jambo la Ardhi katika kata
hiyo kwa kipindi cha muda mrefu sasa huku mahakama ilishakwisha kutoa hukumu
kuwa maeneo hayo ni mali ya wananchi.
Akizungumza
kwenye kikao hicho katibu wa wananchi wa winde Athumani Mkwasi alisema kuwa
ujio wa MNEC huyo katika kijiji hicho umekuwa ni ukombozi mkubwa kwa wananchi
wa eneo hilo kutokana na kunyanyasika muda mrefu huku kesi ya maeneo hayo
yalikwisha kumalizwa na mahakama miaka mingi iliyopita kwani ni tangu enzi za
mababu.
“Ujio wako
katika kijiji hiki ni sawa na kumuona Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli
asiyependa kuwaona wananchi wake wanyonge wakiteseka kwa kitu
ambacho wenye fedha wakinufaika”Alisema.
Aliongeza
kuwa mgogoro huo wa ardhi umekuwa ni kama kuwanyanyasa wananchi kulingana na
kuwa kesi ya eneo hilo ilikwisha malizika na kuamuliwa wananchi kukaa katika
maeneo hayo bila kubuguziwa, mbali na hilo amemuomba MNEC kupeleka ombi la
wananchi wa winde kwa Rais kuwa watendaji wa idara ya ardhi katika wilaya ya
Bagamoyo ni tatizo kubwa na ndio chanzo cha migogoro mikubwa katika sekta hiyo.
Naye zunaiya
Mazige amewapongeza viongozi wa CCM walitembelea eneo hilo ili kujionea
changamoto ambazo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakizipata kwa muda mrefu
kutoka kwa watu wa winde na bhaharesa juu ya malipo kwa kutokuwalipa stahiki
zao na kuwapatia maeneo ya kuishi.
Aliongeza
kuwa hatuna ytatizo la kupisha kwa mradi wa kiwanda cha sukari ila shida kubwa
yetu ni kutokulipwa sitahiki zetu na kuonyeshwa maeneo yetu ya kujenga na
kingine ni ulipwaji mdogo usioendana na usawa wa maeneo yetu.
Akijibu
changamoto hizo za wananchi hao MNEC Haji Jumaa aliwataka wananchi wa eneo
hilo kuwa na subra kwani serikali ya awamu ya tano ni kwa ajili ya wananchi
wanyonge waliokuwa wakinyanyaswa na matajiri kipindi cha nyuma.
Aliongeza
kuwa tatizo lao amelichukua na amewahakikishia kuwa atahakikisha anawaletea
waziri wa Ardhi William Lukuvu ili aweze kuwasaidia na kuwatatulia changamoto
zao za muda mrefu.
Aidha Jumaa
amewapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kuwa na uvumilivu hivyo amewataka kuwa
na uvumilivu huo huo mpaka pale tatizo lao litakapokamilika,ila wale
walioshinda ile kesi waendelee na ujenzi katika maeneo hayo kwani kutokana na
hukumu hiyo hilo eneo ni mali yao.
MNEC wa mkoa wa pwani Haji
Jumaa akipokea hukumu iliyotolewa na mahakama miaka hiyo kutoka kwa katibu wa
wananchi wa winde.
MNEC wa mkoa wa pwani Haji
Jumaa akionyeshwa ramani ya eneo hilo na
wananchi wa kata hiyo ili kutambua mipaka ya maeneo yao.
Wananchi wa kijiji cha
winde kata ya makulunge wakitoa changamoto zao mbele ya viongozi wa CCM
kilichokuwa kikiongozwa na mjumbe wa Nec mkoa wa pwani.
No comments:
Post a Comment