Monday, February 20, 2023

SERIKALI KUJENGA VETA KILA WILAYA.

 No description available.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo.

........................................................................

Na Athumani Shomari.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan itajenga vyuo vya VETA katika kila wilaya nchini.

Waziri, Prof. Mkenda aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika ziara aliyoifanya Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, ambapo alisema Rais Samia tayari ameilekeza Wizara ya Elimu kuwa, kila wilaya iwe na chuo cha VETA.

Alisema tayari wizara ya elimu imejipanga kutekeleza maelekezo ya Rais samia ya kujenga chuo cha VETA kila wilaya ambapo wilaya zote 64 zitajengwa kwa mkupuo pamoja na kimoja kitakachojengwa mkoani Sngwe.

Prof Adolf Mkenda, aliyasema hayo kufuatia ombi la Mbunge wa Bagamoyo, Muharam Mkenge aliyemuomba Waziri huyo wa Elimu kujenga chuo cha VETA katika jimbo la Bagamoyo ili vijana wa Bagamoyo waweze kujifunza fani mbalimbali katika chuo hicho.

Mkenge alisema kwa sasa Bagamoyo inakuwa kwa kasi katika uwekezaji wa viwanda na kutoa fursa mbalimbali kwa vijana wazawa wenye ujuzi wa fani mbalimbali na kuongeza kuwa fursa hizo hazitakuwa na faida kwa vijana wa Bagamoyo ikiwa hawatakuwa na ujuzi wa fani yoyote.

Aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika soko la ajira hivyo uwepo wa chuo cha VETA chenye kutoa ujuzi wa aina mbalimbali kutasaidia kwaa vijana wa Bagamoyo kukabiliana na ushindani katika soko la ajira na kufaidika na uwekezaji unaofanyika katika jimbo hilo.

Alisema tayari mchakato wa kupata eneo la kujenga chuo hicho kwa Bagamoyo umeshakamilika na kupata eneo lenye ukubwa ekari 38 ambzo zitatumika kujenga chuo cha VETA.

Aidha, Mbunge Muharam Mkenge alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuelekeza fedha za elimu katika jimbo la Bagamoyo hali iliyopelekea kuanzishwa kwa shule mpya za sekondari ambazo zimesaidia kuwapungzia watoto kwenda umbali mrefu kufika shuleni.

No description available.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, akizungumza mbele ya Waziri wa Elimu, katika Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo.

No description available.No description available.

 Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala wa ADEM, Dkt. Emanuel Molel, wa pili kulia ni Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu, Bw. Manori Venance, na watatu kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ADEM, Dkt. Naomi Katunzi, kutoka kushoto wa kwanza ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib Okash, na watatu kushoto ni Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Masanja.

 No description available.

No description available.

 

Saturday, February 18, 2023

WAZIRI WA ELIMU AKEMEA WIZI WA MITIHANI.

 No description available.

No description available.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, february 17, 2023.

................................................................


Na Athumani Shomari.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amesema serikali haitafumbia macho wale wote watakaojihusisha na kuvujisha mitihani kwa namna yoyote ile.

 

Waziri Mkenda aliyasema hayo February 17, 2023 alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo  ambapo alisema kitendo cha kuiba au kuvujisha mitihani ni kitendo cha dhulma dhidi ya wale wanaojituma kufanya mitihani kwa akili zao.

 

Alisema tayari baadhi ya watu walioripotiwa kujihusisha na wizi wa mitihani wameshaanza kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa na jeshi la polisi na kuanza kuwahojiwa.

 

Prof. Mkenda amewapongeza polisi nchini kwa kufuatilia matukio ya wizi wa mitihani na wahusika kuwachukulia hatua na kuongeza kwa kusema kuwa, jeshi la polisi nchini linafanya kazi nzuri sana katika kuhakikisha wizi mitihani unakomeshwa.

 

Aliongeza kwa kusema kuwa, walimu wanapaswa kuwa na maadili mema ikiwa ni pamoja na kujizuia kabisa na vitendo vya udanganyifu, wizi au kuvujisha mitihani kwa lengo la kujenga Taifa lenye watu wenye nidhamu, na taaluma iliyopatikana kwa njia sahihi.

 

Waziri Mkenda ameutaka uongozi wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kufundisha maadili pamoja malezi kwa walimu wote watakaosomea uongozi wa elimu ili watakaporudi kwenye shule zao wakasimamie maadili shuleni kwao kwa walimu walio chini yao pamoja na wanafunzi wao.

 

Akizungumza mbele ya Waziri wa elimu, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib alisema kasi ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na ile wanafunzi wa kidato cha kwanza kuripoti shuleni inaendelea vizuri katika wilaya hiyo na kwamba mpaka sasa wanafunzi wote walioripoti ni asilimia 98.

 

Mkuu huyo wa wilaya alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Huluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu hali iliyopelekea wanafunzi wote katika wilaya hiyo kupata vyumba vya madarasa kwaajili ya kusoema.

 

Awali akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ADEM mbele ya waziri, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Masanja, amesema ADEM ina majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa viongozi na watendaji mbalimbali wa elimu katika ngazi zote ikwemo Shule, Kata, Halmashauri, Mkoa, na Wizara.

 

Dkt. Masanja aliongeza kuwa, jukumu linguine ni kufanya tafiti katika maeneo ya uongozi na usimamizi wa elimu ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wake lengo likiwa ni kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya elimu.

 

Aidha, Dkt. Masanja alimueleza Waziri wa Elimu, kuwa kozi za muda mrefu zinazotelewa chuoni hapo ni 

 

1.   Astashahada ya Uongozi, Usimamizi na Utawala katika Elimu (Certificate in Education Leadership, Management and Administration- CELMA) ambayo ni kozi mwaka mmoja na ilianzishwa 2014.

 

2.   Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (Diploma in Education Management and Administration- DEMA) ambapo kozi hii ni ya miaka miwili, na ilianzishwa mwaka 2014.

 

3.   Stashahada ya Udhibiti Ubora wa Shule (Diploma in School Quality Assurance- DSQA) ambayo hapo awali ilijulikana kama Stashahada ya Ukaguzi wa Shule (Diploma in School Inspection-DSI) iliyoanzishwa mwaka 2014.

 

Alibainisha kuwa, katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 jumla ya walimu 4,895 wamehitimu mafunzo ya Stashahada za Uongozi, Usimamizi na Udhibiti Ubora wa Elimu.

 

Dkt. Masanja alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana ADEM inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo.

 

1.   Ufinyu wa bajeti ya kuendeshea mafunzo ya muda mfupi na watendajina viongozi wa Elimu wanaoteuliwa wakiwemo Maafisa Elimu, Maafisa Elimu Kata, Walimu wakuu, Wakuu wa shule na Wadhibiti Ubora wa shule.

 

2.   Baadhi ya Walimu waliochaguliwa kujiunga na masomo yatolewayo na ADEM kukosa ruhusa ya masomo kutoka kwa waajiri wao.

 

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM, ulianzishwa Tarehe 31 Agosti 2001kwa mujibu wa Sheria ya Bunge sura 245. Ambapo kabla ya hapo Chuo hicho kiliitwa Taasisi ya MANTEP (Management Training for Educational Personnel) ambayo ilianzishwa mwaka 1978 na katika kipindi hicho Taasisi ya MANTEP ilijihusisha na utoaji wa Mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa Elimu ya muda mfupi na muda mrefu kwa viongozi na watendaji wa sekta ya elimu. 

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, katika viwanja vya ADEM.

No description available. 

Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala wa ADEM, Dkt. Emanuel Molel, (kulia) akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipowasili katika viwanja vya ADEM.

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akisalimiana Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipowasili katika viwanja vya ADEM.

No description available.

  No description available. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akiangalia machaapisho yanayo onesha kazi za ADEM mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ADEM, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.

No description available. 

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo cha ADEM Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo hicho Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.

No description available. 

No description available.

Viongozi wa Elimu Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo, Watumishi wa Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa pamoja wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea chuo cha ADEM Bagamoyo jana Februry 17, 2023.

No description available. 

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akimkabidhi Waziri wa Elimu, Taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya ADEM na machapisho mbalimbali yanayo onesha kazi za ADEM kwa ujumla.

No description available.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri- ADEM, Dkt. Naomi Katunzi (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt za ADEM, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kushoto)

No description available. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akijaribu zawadi ya T-shirt aliyopewa na uongozi wa ADEM, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.

No description available.

No description available.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, anaeshuhudia (katika) ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.

No description available. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, (kushoto).