Posts

Showing posts from September, 2019

ACT. WAZALENDO YAWASILISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA KESI YA KATIBA.

Image
Na Karama Kenyunko CHAMA cha ACT- Wazalendo kupitia bodi yake ya dhamini, wamewasilisha maombi ya kujiunga katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mkulima Dezydelius Patrick Mgoya, ambaye anahoji kuwepo kwa kikomo cha urais nchini. Maombi hayo yamebainishwa leo Septemba 30, 2019 na Jaji Kiongozi wa mahakama hiyo, Dk Eliezer Feleshi, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na maelekezo maalumu ya namna ya usikilizwaji wa pingamizi la awali la Seriali dhidi ya kesi ji Kiongozi Dk Feleshi ndiye kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo. Wengine katika kesi hiyo ni Dk. Benhajj Masoud na Seif Kulita. Katika maombi hayo, ACT inayowakilishwa na kampuni ya uwakili ya Law Guards Advocates wamewasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura, wakiomba maombi yao yasikilizwe haraka. Kufuatia maombi hayo, mahakama imesimamisha usikilizwaji wa kesi ya msingi na kuamua kusikiliza kwanza maombi hayo ya ACT-Wazalendo. Jaji Feleshi ambae anaongoza jopo la ma...

VIJANA MAPINGA BAGAMOYO WATAKIWA WASIWE CHANZO CHA MPASUKA.

Image
Kaimu Katibu Uvccm Bagamoyo ndugu Omary Ally amewasihi Vijana kuwa wavumilivu hasa Katika kipindi hiki cha Uchaguzi ili kuepusha Migongano ndani ya Chama yenye kuleta Mipasuko ambayo Miaka yote ndio imewanufaisha Vyama vya upinzani kwenye Chaguzi. Katibu huyo ameyasema hayo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni wa heshima kwenye hafla ya kuwapongeza Vijana wa kata ya Mapinga waliohitimu Mafunzo ya Ujasiriamali Katika Kambi maalum ya Vijana wilayani humo iliyofanyika kwa siku 10. Pamoja na hayo Ndugu Omary Aliwataka Vijana hao kutembea Kifua mbele kwakua Serikali ya awamu ya Tano imefanya Mengi Makubwa katika kuleta maendeleo nchini na yote yanaonekana hivyo kila wanapokaa basi wayaseme mafanikio hayo. “Ndugu zangu Nchi yetu kwa Sasa inaongoza miongoni mwa nchi za kusini mwaAfrika Katika kupambana na Umasikini na jitihada hizi zinachochewa sana na Kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli hivyo tuendelee kumuombea Rais wetu Kwani Sasa Taifa letu limep...

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA DPP KUHUSU WAHUJUMU UCHUMI.

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga katika picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30,2019. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw.Biswalo Mganga baada ya kupiga naye picha ya pamoj...