MAHAFALI YA TISA YEMEN SECONDARY SCHOOL 2017.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya shule za Yemen Hassan Akrabi, katikati ni Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Baraza la wakuu wa shule za Kiislamu Tanzania, Ansaar Abubakar Kachwamba na kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Yemen, mwalimu Hamisi Togwa. Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Baraza la wakuu wa shule za Kiislamu Tanzania, Ansaar Abubakar Kachwamba akizungumza katika mahafali hayo ya tisa yaliyofanika viwanja vya shule za Yemen Chang'ombe jijini Dar es Salaam. ............................... Vijana wanaohitimu katika shule za kiislamu hapa nchini wametakiwa kuendeleza maadili mema waliyopata katika shule hizo ili kuujengea heshima uislamu. Akizungumza katika mahafali ya tisa ya shule ya sekondari Yemen, Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Ansar Abubakar Kachwamba alisema jamii imejenga imani kubwa kwa shule za kiislamu na waislamu kwa ujumla hivyo ni ju...