Posts

Showing posts from May, 2017

SERIKALI KUENDELEA KUPAMBANA NA KILIMO CHA MIRUNGI

Image
Serikali imetangaza kuendesha operesheni ya kuteketeza mashamba ya mirungi kote nchini ikiwa ni mkakati wa kupambana na dawa za kulevya. Hatua hiyo inafuata baada ya kuteketeza mashamba ya bangi zaidi ya 150 yenye ukubwa wa ekari 165 katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Sianga wakati akizungumza kwenye kipindi maalum kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV. “Dawa za kulevya zinaathiri sana nguvu kazi ya Taifa na tangu Mamlaka hii imeanza tumefanikiwa kudhibiti uingizaji wa Heroine, Cocaine na dawa nyingine za kulevya na tumewakamata wafanyabiashara wakubwa ambao walikuwa wanatafutwa na mataifa makubwa na hiyo ni hatua kubwa kwa nchi yetu katika mapambano haya” Alisisitiza Sianga. Akifafanua Sianga alisema kuwa Serikali imepanga kuongeza vituo vya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya katika Mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza kwa awamu ya ...

TAARIFA KWA WAKAZI WA WILAYA YA BAGAMOYO.

Image

IGP SIRRO AANZA KUSHUGHULIKIA MAUAJI MKOANI PWANI.

Image
Mkuu wa jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za  kudhibiti masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya waandishi wa habari pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza IGP Mpya, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam ............................ Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro ameahidi kutoa sh.milion 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kufanikisha kuwakamata watu wanaofanya mauaji ya viongozi huko Kibiti wilayani Rufiji Utete mkoani Pwani. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sirro amesema kumekuwa na mauaji ya wananchi na Askari katika Wilaya ya Rufiji Utete pamoja na Wilaya ya Mkuranga ambayo yamekuwa yakifanywa na wahalifu wachache kwa malengo wanayoyajua wao. Amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na Operesheni mbalimbali kuhakikish...

MAGAZETI YA LEO 31 MAY 2017.

Image

WAHARIRI HABARI WAPEWA SEMINA.

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii. Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii.   Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya...