Kamanda wa polisi
mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa akielezea
msako endelevu unaendelea mkoani humo huku akieleza kauli mbiu yake ya Tindua
Tindua hadi kieleweke. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Kamanda wa polisi
mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa akionyesha
baadhi ya luninga flat screen zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mmoja wa watu walioibiwa luninga zao, mzee Lebul
Mfinanga (wa kulia aliyebeba luninga) akiwa ametoka kutambua luninga yake makao
makuu ya polisi Pwani .
Picha na Mwamvua Mwinyi
...................................................
Na Mwamvua
Mwinyi, Pwani
JESHI la
polisi mkoani Pwani, limekamata luninga kumi flat screen zenye thamani ya sh.
mil.18, ambazo ziliibiwa katika matukio mbalimbali ya uvunjaji, mkoani
humo.
Aidha
linamshikilia mtu mmoja jina limehifadhiwa baada ya kukumatwa akiwa na madumu
kumi yenye ujazo wa lita 20 ya mafuta aina ya dizeli ,aliyoiba katika
mradi wa ujenzi wa reli ya standard gauge , Soga wilaya ya kipolisi
Mlandizi.
Akithibitisha
kutokea kwa matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo
Nyigesa alisema, wanashikilia watu nane kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio
hayo.
Nyigesa
alieleza katika msako huo wamekamata jenereta mbili kubwa zenye thamani ya
milioni 6.5 ambazo ni aina ya Euro power EP. 6500E na boss BG -2500 .
Alifafanua,
vitu vingine vilivyokamatwa ni deki mbili, vingamuzi viwili, speaker mbili,
music system mbili, home fieta moja, rimoti sita, speaker twiter mbili, flash
moja kapeti za chini ya sakafu mbili, stendi ya vyombo moja na extention moja.
Hata hivyo
kamanda huyo alisema , mtuhumiwa aliyekamatwa kijiji cha Mperamumbi akiwa
amepakia mafuta kwenye pikipiki aina ya sanlg namba MC. 197 BJD kutoka mradi wa
standard gauge wanamhoji na atafikishwa mahakamani.
Katika
tukio jingine wamekamata pikipiki saba na bangi kiroba kimoja kilichokuwa
kinasafirishwa kwenda kuuzwa.
Nyigesa
alibainisha, katika tukio hilo mmiliki wa pikipiki yenye namba za usajili MC
951 BSA anaombwa kujisalimisha mwenyewe kituo chochote cha polisi ndani
ya siku tatu vinginevyo watamsaka popote ili kueleza kuhusu bangi
hiyo.
“Sisi
wakati tukiwa kwenye hapa kazi tuu, wao wapo kwenye wizi tuu, tunawapa salamu
wakati wengine wakifyekelea mbali, kwa sisi mkoa wa Pwani tunaendelea na
operesheni na msako wa TINDUA TINDUA, tutatindua mpaka kieleweke “alisisitiza
Nyigesa.
Alitoa
wito kwa wananchi kuacha tabia ya kununua vitu mikononi bila ya kupewa risiti
kwani atakaekutwa na mali ya wizi nae atachukuliwa hatua za kisheria.
Nyigesa
aliwaasa pia kuwa ,wabia katika suala la ulinzi shirikishi kwenye maeneo yao
ili kukabiliana na ujambazi, uvunjaji na uhalifu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment