Bilionea Mohammed ‘Mo’ Dewji (kulia) akiwa na
Mdhamini wa klabu ya Simba SC, Ramesh Patel (kushoto) kwenye kikao cha jana Novemba 10, 2018.
......................................
MFANYABIASHARA
Bilionea, Mohammed ‘Mo’ Dewji amekutana na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo
iliyochaguliwa katika uchaguzi Mkuu wa klabu uliofanyika Novemba 5 mjini Dar es
Salaam.
Kikao hicho kilihusisha viongozi waliomaliza muda wao, chini ya kaimu Rais Salum Abdallah ‘Try Again’ na Mdhamini wa klabu, Ramesh Patel.
Mo Dewji alitambulishwa rasmi Bodi ya Ukurugenzi ya Simba chini ya Mwenyekiti, Swedy Nkwabi na Wajumbe Hussein Kitta Mlinga, Dk. Zawadi Ally Kadunda, Suleiman Haroub Said, Mwina Mohammed Kaduguda na Asha Ramadhani Baraka.
Mo
Dewji, Mbunge wa zamani wa Singida Mjini, kukubali kununua asilimia 49 za hisa
za klabu ya Simba SC kulingana na maelekezo ya Serikali badala ya asilimia 51
alizotaka yeye awali katika mkutano Desemba 3, mwaka jana, ambao uliazimia
kumfanya mwanahisa mkuu wa klabu katika mfumo mpya wa uendeshwaji.
Mo pekee aliweka dau la Sh Bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada ya
klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa Sh. Bilioni 20 miezi miwili
iliyopita, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia
49 kwa mtu mmoja.
Wanachama 1320 walihudhuria mkutano huo wa Desemba 3, mwaka jana kutoka Dar
es Salaam na mikoa jirani na kwa furaha ya ushindi huo, Mo Dewji alitoa ahadi
10 za kuleta mabadiliko makubwa, ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mazoezi wa nyasi
za asili na nyasi bandia pamoja na hosteli ya kisasa ya wachezaji.
Na
uchaguzi wa Jumapili iliyopita Simba SC ulifanyika baada ya uongozi uliopita
ulioingia madarakani juni 30, mwaka 2014 chini ya Rais, Evans Elieza Aveva,
Makamu wa Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Wajumbe Iddi Kajuna, Said Tully,
Collins Frisch, Ally Suru na Jasmine Badour kumaliza muda wake.
Lakini Aveva na Kaburu hawakufanikiwa kumalizia muda wao madarakani,
kufuatia kuwekwa rumande katika gereza la Keko tangu Juni 29, mwaka jana kwa
tuhuma za kughushi nyaraka, kesi ambayo bado inaendelea katika Mahakama ya
Kisutu mjini Dar es Salaam.
Na Julai 1, mwaka jana, Kamati ya Utendaji iliwateua ‘Try Again’ na Iddi
Kajuna kukaimu nafasi za Aveva na Kaburu na hao ndiyo waliosimamia mchakato
mzima wa mabadiliko ya klabu kuelekea uchaguzi huo.
Nkwabi
ambaye amekidhi matakwa ya Katiba mpya ya Simba SC kuwa na elimu ya Shahada sasa
ataongoza Bodi ya Wakurugenzi itakayokuwa na Wajumbe wanane chini yake huku
akiwa na mamlaka ya kuteua Wajumbe wengine wanne, kati yao mmoja lazima awe
mwanamke ili kukamilisha Bodi ya Ukurugenzi ya watu wanane.
Aidha, Mo Dewji anakutana na Bodi ya Ukurugenzi ya klabu siku moja tu baada
ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutaja ratiba ya michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika msimu wa 2018- 2019, Simba ikipangiwa kuanza na Mbabane
Swallows Swaziland katika Raundi ya Awali ya mchujo.
Na
Wekundu wa Msimbazi, wakifanikiwa kuvuka mtihani huo, watakwenda hatua ya
mwisho ya mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo, ambako
watamenyana na mshindi kati ya Uniao Desportiva Do Songo ya Msumbiji na Nkana
FC ya Zambia, anayochezea beki wake wa zamani, Mtanzania, Hassan Kessy
aliyewahi kucheza na Yanga pia.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC na
viongozi waliomaliza muda wao katika kikao cha leo
No comments:
Post a Comment