Posts

Showing posts from September, 2024

TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA MKAZI ILI TUPIGE KURA. RC LINDI

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 11 hadi 20, 2024 na upigaji wa kura 27, Novemba 2024 kuchagua viongozi wa serikali za Mitaa. "Niwaombe vijana wote, niwaombe akina mama, akina Baba tuende tukajiandikishe kwenye daftari la mkazi ili tukaweze kupiga kura "  Wito huo ameutoa leo tarehe 29 septemba 2024  katika viwanja vya Kilwa Kivinje ambako kivinje Jogging klabu wameandaa bonanza lakualika klabu mbalimbali kutoka maeneo na mikoa mbalimbali kama vile Dodoma, Mtwara, Pwani na Dar Es Salaam lenye lengo la kudumisha afya, ushirikiano, upendo, umoja na hamasa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba 27, 2024. Mhe. Zainabu Telack ametoa angalizo kwa wananchi ambao hawana taarifa sahihi kuhusu vitambulisho walivbyo navyo na zoezi la kujiandikisha katika daftari la mkazi. ...

RAIS DKT. SAMIA AHITIMISHA ZIARA YA SIKU SITA RUVUMA.

Image
  Awashukuru wananchi ushirikiano wao, ajivunia mafanikio makubwa utekelezaji wa Ilani ya CCM. Asisitiza wananchi kujiandikisha Uchaguzi Serikaki za Mitaa. Mhe. Rais Dkt. Samia amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi takriban elfu 50, katika Uwanja wa kihistoria, wa Kumbukumbu ya Majimaji, mjini Songea,  tarehe 28 Septemba 2024. Katika hotuba yake mbele ya umati mkubwa wa watu waliofurika kumsikiliza Rais Dkt. Samia, pamoja na masuala mengine, ameendelea kusisitiza wito wake kwa Watanzania wenye sifa kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuanzia ratiba ya kujiandikisha kupiga kura iliyopangwa kuanza Oktoba 11 - 20, mwaka huu.  Rais Dkt. Samia ametumia mkutano huo pia, kuendelea kuwashukuru Watanzania wanavyoshirikiana na Serikali ya CCM, chini ya uongozi wake, hali ambayo imesaidia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kwa mafanikio makubwa hadi sasa, katik...

HAKIMU, WAKILI WA SERIKALI WAJA JUU WAKILI CHUWA KUCHELEWESHA KESI.

Image
  Na Mwandishi Wetu HAKIMU Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Aaron Lyamuya, ameelezea kukerwa na tabia ya wakili wa utetezi kwenye kesi ya jinai, Edward Chuwa kutaka kesi iahirishwe mara kwa mara. "Hivi siyo vitu vya kutengeneza vipo kwenye rekodi za mahakama, hili shauri lazima liishe hatuwezi kuja hapa kila siku tunakaa tu hatuna cha kufanya hapa,  kuna polisi, kuna karani na mawakili wapo tu kila siku kuahirisha kesi hapana, “ alisema Lyamuya Kesi hiyo ya tuhuma za kujeruhi na kutoa lugha ya matusi inawakabili wanandoa Bharat Nathwan (57) na Sangita Bharat (54)  ambapo nathwani anatuhumiwa kuwa Julai 21,2023 akiwa eneo la mtaa wa Mrima-Kisutu, jengo la Lohana, ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam alimsababishia madhara makubwa Kiran Lalit kwa kuzamisha kichwa chake kwenye ndoo la saruji iliyochanganywa. Hakimu Lyamuya alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba analipwa kwa hiyo anatakiwa kufanya kazi na pia Wakili wa Serikali analipwa anatakiwa...

RAIS SAMIA AFUNGUA BARABARA YA MBINGA - MBAMBA BAY (KM 66) - RUVUMA

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua barabara  ya Mbinga - Mbamba Bay yenye urefu wa kilometa 66 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Ruvuma, Septemba 25, 2024. Ujenzi wa Barabara ya Mbinga - Mbamba Bay (km 66) umesimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara - TANROADS chini ya Mkandarasi China Henan International Cooperation Group Co. Ltd kutoka China na Mhandisi Mshauri kutoka SMEC International Pty Ltd kutoka Australia kwa gharama ya Shilingi Bilioni 122.76. Katika utekelezaji wa barabara hiyo, Kiasi cha shilingi Milioni 637.4 kilitumika kulipa fidia kwa wananchi walioathirika na ujenzi kwa mujibu wa sheria. Barabara ya Mbinga - Mbamba Bay ni sehemu ya barabara kuu ya ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor) yenye jumla ya urefu wa kilometa 826 inayoanzia Mtwara mpaka Mbamba Bay ambapo pia barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Mtwara pamoja na Mkoa wa Mbeya na nchi Jirani ya Malawi kupiti...

JKCI YAENDELEA KUWA LULU UTALII TIBA AFRIKA

Image
  Madaktari wake waitwa Zambia kufanya upasuaji wa moyo Na Mwandishi Wetu   Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya umeendelea kuipaisha Tanzania ambapo sasa madakati bingwa wanne wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI wako nchini Zambia wakiendelea  kufanya upasuaji wa moyo. Timu hiyo ya madakari hao itashirikiana na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya Zambia na watafanyakazi upasuaji wa moyo kwa muda wa wiki moja . Mkuu wa ujumbe huo, Dk Viviane Mlawi wa (JKCI),  ambaye ni daktari bingwa wa moyo kwa watoto, alisema  ujumbe huo pia umeambatana na mtaalam mbobezi wa chumba cha upasuaji na mtaalamu wa usingizi katika upasuaji Moyo. Alisema wameambatana pia na mbobezi katika  kuhudumia wagonjwa wa nje wanaokuja kupata matibabu Tanzania,  Dk. Maiyer Msengi na wauguzi wawili ambao ni wabobezi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Dk Mlawi alisema malengo makubwa ya safari hiyo  ni matano ambayo ni kufanya u...

MAJID MWANGA AZINDUA SAMIA BODABODA DAY, MLELE.

Image
  Tarehe 23 September 2024 imekuwa ni siku ya neema na kukumbukwa kwa maafisa usafirishaji wa wilaya ya Mlele maarufu Kama bodaboda hii ni baada ya Ofisi ya mkuu wa wilaya ya mlele chini ya mkuu wa wilaya Mh Alhaj Majid mwanga kuandaa siku maalumu ya SAMIA BODABODA DAY iliyo fanyika halmashauri ya mlele shule ya msingi inyonga na kupambwa na kauli mbiu ya MIMI NI KIJANA WA SAMIA "nitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa November 27/ 2024 Siku hiyo maalumu ya boda boda Samia day imeyakutanisha makundi yote ya BODABODA kutoka pande zote za halmashauri ya mlele na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali Kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mlele BI SIGILINDA MDEMU, Pia Wakuu mbalimbali wa taasisi, akiwemo mkuu wa kitengo cha usalama barabarani ambae alipata wasaa wa kutoa nasaha kwa madereva hawa wa bodaboda na kuwaasa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali mbazo zimekuwa zkijitokeza mara kwa mara kutokana na uzembe. Akizungumza katika si...

SERIKALI YAIPONGEZA GREEN ACRES KWA KUENDELEA NA KUFANYA VIZURI KITAALUMA.

Image
  Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeipongeza shule ya msingi na sekondari, Green Acres ya jijini Dar es Salaam kwa namna ambavyo imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya Wilaya hadi taifa. Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu wa Wizara ya Elimu,  Sayansi na Teknolojia, Victor George, wakati wa mahafali ya 24 ya  shule hiyo  yaliyohusisha wanafunzi wa awali, msingi na sekondari. “Nawapongeza sana kwa kuendelea kufanya vizuri kitaaluma na nawashauri muendelee kuwekeza kwa wanafunzi hawa maana bila hivyo hatuwezi kuwa na taifa bora la kesho na mmeweka miundombonu mizuri ambayo inawawezesha kusoma kwa utulivu,” alisema. Alisema serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele kwenye kuwekeza kwenye ngazi zote za  elimu kuanzia awali, msingi sekondari, vyuo vikuu vikuu vya kati ili watoto wanaopata fursa ya kwenda huko kupata elimu bora. “Vijana huu ni mwanzo tu wa safari ndefu ya maisha, msione mmefi...

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MTYANGIMBOLE KWA NIABA YA MIRADI 30 YA MAJI MKOA WA RUVUMA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan leo September 24,2023 ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Mtyangimbole Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma kwa niaba ya Miradi 30 ya Maji inayotekelezwa Mkoani humo. Mradi wa tank la Maji Mtyangimbole una uwezo wa kupokea Lita milioni 1.9 na utahudumia Wananchi takribani 14,000.