Tuesday, November 13, 2018

WAFUGAJI KUFANYA UCHAGUZI NOVEMBA 30

Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ya Chama Cha Wafugaji Tanzania, Veronica Ndetieai (kushoto) akinukuu maombo muhimu katika kikao na waandishi wa Habari kuzungumzia uchaguzi wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika Novemba 30, 2018.
......................................................

Na Omary Mngindo, Dakawa

CHAMA Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), kinataraji kufanya uchaguzi wa viongozi wake wa Kitaifa, unaotarajiwa kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu, mkoani Dodoma.

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Veronica Ndetiai Mwenyekiti wa Tume wa chama hicho, alipozungumza na waandishi wa habari katika Mnara wa kumbukumbu ya Edward Sokoine, Kijiji cha Sokoine, Kata ya Dakawa wilaya ya Mvomelo mkoani Morogoro.

Ndetiai alisema kuwa fomu za kuwania nafasi mbalimbali zimeanza kutolewa Ijumaa ya Nov 9, huku akiwahimiza wanachama kuchangamkia uchukuaji wa fomu hizo, ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kama ilivyopangwa.

"Nafasi zitazowaniwa kwenye uchaguzi huo unaoyaraji kufanyika mkoani Dodoma ni Mwenyekiti, Makamu, Katibu Mkuu ma Msaisizi wake, Mhasibu na Wajumbe wa Kamati Tendaji," ilieleza taarifa hiyo.

Aidha tarifa ya Ndetiai imetaja sifa za wanachama ikiwa ni pamoja na kuwa mwanachama hai Kikatiba, ajeu kusoma na kuandika, mwenendo mzuri kitabia na anayekubalika, awe tayari kujitolea.

"Awe mvumilivu, msikivu na mwenye uwezo wa kutetea na kulinda maslahi ya Chama kwa uadilifu mkubwa, Katibu awe na uwezo wa kuongoza wengine," ilieleza sehemu ya taatifa hiyo.

Taarifa hiyo ikizungunzia nafasi ya Mtunza fedha, imeelezea kwa awe na uwezo wa kutunza kumbukumbu na vitabu vya fedha, mwajibikaji, mwaminifu
na ikibidi awe na taaluma ya fedha.

Ndetiai imeongeza kuwa alisema kuwa chama hicho kilichoanzishwa rasmi mwaka 2013, na kupatiwa usajili namba S.A 19186 kikiwa na malengo ya kuunganisha Wafugaji wote wa Tanzania Bara na Visiwani.

No comments:

Post a Comment