Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga
Hasunga (Mb) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda leo
Novemba 13, 2018 mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa
ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza
ununuzi. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
.................................
Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo,
Mtwara
…………………………………………………………………………………………………
Ikiwa ni siku moja tu mara
baada ya kuapishwa kuongoza wizara ya kilimo katika hafla iliyofanyika Ikulu
Jijini Dar es salaam Jana Jumatatu Novemba 12, 2018, Waziri wa kilimo Mhe Japhet
Ngailonga Hasunga (Mb) Leo Tarehe 13 Novemba 2018 ameongoza viongozi wakuu wa
Wizara yake kutembelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya
kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu.
Katika msafara huo Waziri
Hasunga atatembelea Mkoani Mtwara ambapo ameambatana na Naibu Waziri wa kilimo
Mhe Innocent Lugha Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe
watakaotembelea Mkoa wa Lindi, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof
Siza Tumbo atakayetembelea Mkoa wa Ruvuma.
Katika ziara hiyo viongozi
hao wakuu watahakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa naBodi ya
usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la
wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.
Vilevile watahakiki taarifa
za Ubora wa maghala kama zilivyopitishwa na
Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (Warehouse Receipt Regulatory
Board-WRRB) pamoja na Ubora wa ghala.
Watahakiki uwezo wa
maghala na kiasi kilichopo ghalani, na kuhakikisha taarifa ya umiliki wa Korosho
zilizopo kwenye ghala.
Aidha, viongozi hao
watahakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya
Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na
kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya
ghala (Warehouse Report).
Katika ziara hiyo timu ya
viongozi wakuu kutoka wizara ya kilimo wataambatana pia na Ofisini za Wakuu wa
Mikoa na Wilaya, Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT),
Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania
(TARI)-Naliendele, na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (WRRB).
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga
Hasunga (Mb) akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe
Gelasius Byakanwa leo Novemba 13, 2018, mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa
ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu
kabla ya kuanza ununuzi.
Naibu waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa (Mb) akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa
ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza
ununuzi. Mwingine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda, leo
Novemba 13, 2018.
Kulia ni katibu Mkuu wa wizara ya kilimo
Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo
walipowasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho
zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi leo Novemba 13, 2018.
No comments:
Post a Comment