Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa
Geita kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. Kulia ni
Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
.................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Wakuu wa
Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wahakikishe wanasimamia
vizuri uwajibikaji na utowaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yao bila ya woga.
Kadhalika, Waziri Mkuu amemtaka kila mtumishi wa
umma nchini awajibike katika kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu
ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhilifu,
wavivu na haitosita kuwachukulia hatua.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza
na watumishi, viongozi wa mkoa, wilaya ya Geita na taasisi za umma katika
mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mji Geita.
“Watumishi
fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya,
ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”
Waziri
Mkuu aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia
sheria na kanuni za kazi na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni
kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza watumishi wa umma hususani Wakuu wa
Idara wahakikishe wanakuwa na kitabu cha Ilani ya Uchanguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ili wapate muelekeo wa utekelezaji washughuli zao.
Waziri
Mkuu amesema kitabu cha Ilani ya uchanguzi cha CCM 2015/2020 kina maelekezo ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kila idara inatakiwa kuangalia
maelekezo yaliyotolewa kuhusu idara husika na kuyafanyia kazi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alimuhakikishia
Waziri Mkuu kwamba yeye kwa kushirikiana na viongozi wenzake watayafanyia kazi
maelekezo yote ambayo ameyatoa.
Baadhi
ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo,
Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo,
Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment