Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi Theresia Mmbando, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 33 la kisayansi pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha wanasansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT), mjini Bagamoyo, pembeni yake ni Rais MeLSAT, Yahya Mnung'a.
..................................
Waajiri
katika sekta ya Afya Mkoani Pwani, wametakiwa kuajiri wataalamu wa Maabara
za Afya, waliosomea kazi hiyo ili kupata matokeo mazuri ya vipimo vya magonjwa na tafiti
mbalimbali.
Wito
huo umetolewa mjini Bagamoyo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo,
katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi
Theresia Mmbando wakati wa kufungua
Kongamano la 33 la kisayansi pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha
wanasansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT).
Amesema
matokeo ya wataalamu wa maabara za Afya ndio yanayoweza kuleta mafanikio katika kutatua
tatizo iwe ni ugonjwa ama utafiti wa aina mbalimbali.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, ni vyema sasa waajiri binafsi na serikali kuhakikisha
wanaajiri wataalamu wa Maabara za Afya wenye sifa ili kuepuka kupata majibu yasiyo
sahihi wakati wa vipimo.
Aidha,
amewataka wataalamu hao wa maabara za Afya kutumia vifaa vilivyopo kwa usahihi ili waweze
kutoa majibu kwa yaliyo sahihi.
Ametoa
wito pia kwa wataalamu hao kujiunga na Chama cha wanasayansi wa Maabara
za Afya Tanzania (MeLSAT) ili kujadili mambo kwa pamoja na kuweza kuyapatia
ufumbuzi wa kitaalamu.
Awali,
Rais wa Chama cha wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT) Yahya Mnung'a akisoma
hutuba ya chama chao kwa mgeni rasmi, ameiomba serikali kuwepo na kurugenzi ya
Maabara ili kuboresha huduma za uchunguzi na utoaji wa huduma za afya.
Alisema
katika Mkutano wa Shirika la Afya Duniani, uliofanyika Maputo Msumbiji mwaka
2008, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Afya (wakati huo) yapo mambo
waliyokubaliana katika mkutano huo.
Alibainisha
kuwa, miongoni mwa mambo waliyokubaliana ni pamoja na kila nchi mwanachama
ianzishe Kurugenzi ya Maabara ili kuboresha huduma za Uchunguzi na utoaji wa
huduma bora za Afya.
Aidha,
katika hutua nyingine, Mnung'a
alisema wanaishukuru serikali kwa kuendelea
kuimarisha mafunzo ya Maabara za Afya hapa nchini na kuruhusu taasisi binafsi
kutoa mafunzo katika ngazi mbalimbali za taaluma hiyo.
Hata
hivyo, Rais huyo wa MeLSAT alisema lipo tatizo kubwa katika muundo wa mishahara
ya wateknolojia wasaidizi na wanasayansi wa maabara za Afya wa mwaka 2009.
Alisema
kuwa, toka kuanzishwa kwa kozi ya stashahada ya juu ya sayansi za maabara za
Tiba 1993, hakuna muundo na Daraja la mshahara kwa mtaalamu wa maabara
aliyemaliza ngazi hiyo.
Washiriki
wa Kongamano hilo wamesema kukutana kwao kunasaidia kujadili kwa pamoja
changamoto zinazowakabili wataalamu wa maabara za Afya na kuona namna ya kuwasilisha
mapendekezo yao kwa watunga sera.
Kongamano la 33 la Kisayansi limeambatana na
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wa Chama cha wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania
(MeLSAT) ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "Jukumu la Maabara za Afya
katika utoaji wa huduma zilizo bora"
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi Theresia Mmbando, (wa tatu kulia) akiwa meza kuu na viongozi waandamizi wa maabara za Afya nchini katika Kongamano la 33 la kisayansi pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha wanasansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT), mjini Bagamoyo.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi Theresia Mmbando, (wa tatu kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la 33 la kisayansi pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha wanasansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT), mjini Bagamoyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi
Theresia Mmbando, (katikati) akisalimiana na washiriki wa Kongamano la 33 la kisayansi pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha
wanasansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT), mjini Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment