MAAMBUKIZI YA MALARIA KAGERA YAFIKIA ASILIMIA 18.
Na Alodia Babara Bukoba. Misimu miwili ya mvua ya vuli na masika inayonyesha mkoani Kagera imetajwa kama sababu ya mbu kuzaliana na hivyo kusababisha kiwango cha maambukizi ya malaria kufikia asilimia 18, mkoani humo huku kiwango cha taifa kikitajwa kuwa ni asilimia 8. Kufuatia kiwango hicho kuwa juu, wilaya mbili za Karagwe na Kyerwa ambazo ziko pembezoni na vijiji viko umbali wa kuanzia kilomita tano kufika katika vituo vya afya wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 38 wamepewa vifaa tiba. Akizungumza leo Novemba 30,2023 katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kutolea huduma za tiba katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo mkurugenzi wa mradi wa Shinda malaria Dk Dunstan Bishanga amesema wahudumu hao walipewa mafunzo ya awali jinsi ya kupima joto na kuwaelimisha wanachi juu ya matumizi sahihi ya vyandarua. “Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa mitatu hapa nchini yenye maambukizi ya juu ya malaria ambapo watu 18 kati ya watu 100 wameathirika na vimelia vy...