Posts

Showing posts from January, 2019

WASAUDIA WATUA TANZANIA KUTAFUTA FURSA ZA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Wasaudia watafuta Fursa za Kuwekeza katika Viwanda Tanzania Ujumbe wa wawekezaji wa makampuni makubwa 15 ya Saudi Arabia utafanya ziara nchini Tanzania tarehe 30 na 31 Januari 2019 kwa madhumuni ya kuangalia fursa ya kuwekeza kwenye viwanda. Ziar hiyo inatokana na juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Saudi Arabia na wadau wengine  wa kushawishi wafanyabiashara wakubwa kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali. Ujumbe huo wa watu 20, utakapokuwa nchini pamoja na mambo mengine, utashiriki kongamano la biashara litakalofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar Es Salaam tarehe 30 Januari 2019 kuanzia saa mbili asubuhi. Kongamano hilo litafuatiwa na mazungumzo ya ana kwa ana baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Saudi Arabia. Kongamano hilo linaloratibiwa na Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) litatoa fursa kwa wafanyabiashara hao ...

WAZIRI JAFO ATOA WIKI TATU KWA MHANDISI FRANCIS BAGO

Image
Na.Alex Sonna,Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo ametoa wiki tatu kwa mhandisi Francis Bago  anayesimamia ujenzi wa kituo cha Afya cha Mkonze Wilaya ya Dodoma, kuhakikisha kituo hicho kimekamirika. Waziri Jafo ametoa kauli  hiyo leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akikagua miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ndani ya Jiji la Dodoma, amesema ndani ya wiki tatu ujenzi wa kituo hicho uwe umekamirika kwani upo nyuma ya wakati. Amesema huo ni uzembe kuona kituo hicho hakijakamirika kwani kipo Mjini lakini ujenzi wake haujakamirika na unasuasua, wakati vituo vilivyopombali ujenzi wake umekamirika na mgao ulitoka pamoja na wao wapo mwishoni lakini kituo hicho bado sana. “Nashangaa kuona kituo hiki kipo Mjini kabisa ujenzi wake haujakamilika, wakati huo huo kuna vituo vimekamilika na vipo mbali na fulsa na vifaa vya ujenzi vinapatikana kwa umbali mrefu, kwahiyo huu ni uzembe na naagiza ...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BUNGENI LEO

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (katikati) na Fatma Toufiq kwenye viwanja vya Bunge jijjini Dodoma  Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Longido Dkt. Stephen Kiruswa, nje ya jengo la utawata Bungeni jijjini Dodoma  Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)