Mbunge wa TEMEKE (CUF), Abdallah Mtolea amejivua
uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya CUF akidai
kumekuwa na migogoro mingi ndani ya chama chake. Mtolea ametangaza uamuzi huo
bungeni jijini Dodoma hii leo Novemba 15, 2018.
Baada ya kumaliza kutangaza kujiuzulu, Mtolea
alitoka nje ya Ukumbi wa Bunge na kuondoka bungeni hapo.
Taarifa hizo zimethibitishwa pia na Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ambaye amesema amepokea barua
ya kujiuzulu kwake.
Aidha, Mtolea amevikaribisha vyama vingine vya
siasa nchini kufanya naye kazi akidai bado anatamani kuendelea kuwatumikia
wananchi wa Temeke.
No comments:
Post a Comment