Hadija Omary, Lindi.
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Lindi wampongeza Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli
kwa uamuzi wa kununua korosho kwa bei inayomletea tija mkulima.
Akizungumza na waandishi
Wa habari ofisini kwake leo Novemba 13, 2018 Wilayani Nachingwea, Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Lindi,
Majid Lupanda, amesema hatua iliyochukuliwa na Mh. Rais, ni hatua ya kishujaa, na
imeonesha wazi kuwa, ni moja ya mfulululizo wa matendo ya kishujaa yanayofanywa
na Mh. Rais, kwa maslahi mapana ya Taifa, na sio kwa maslahi binafsi.
" Mh. Mh.Rais ameonesha ushujaa mkubwa katika hili, tunampongeza
sana kwa hatua mzuri aliyoichuku ya kununua korosho kwa bei yenye tija kwa
mkulima, na tunamuoba Mungu azidi kumpa nguvu ya kuendelea kuitumikia
Tanzania kwa maslahi mapana ya Taifa " alisema Luponda.
Aidha Lupanda pia
alimpongeza Mh. Rais kwa hatua ya kufufua kiwanda cha kubangua
korosho ikiwa ni mwelekeo wa serikali katika Tanzania ya viwanda pia ni moja ya
njia ya kuongeza pato kwa Taifa na chanzo cha ajira kwa vijana wa kitanzania.
Hata hivyo katika
mazungumzo yake na waandishi wa habari, Mwenyekiti huyo wa uvccm mkoa, alilaani
vikali wanasiasa wanajaribu kurudisha nyuma jitihada za Mh. Rais, katika
kuipambania Tazanzania.
"
Tunajua kuwa Mh. Rais wetu anafanya kazi mzuri sana inayompendeza Mungu, na pia
kuna watu wachache wanaotumika vibaya na wasioitakia mema nchi yetu katika
kuharibu ama kurudisha nyuma jitihada za Mh. Rais katika mapambano ya kuipeleka
mbele nchi yetu kimaendeleo, sisi kama umoja wa vijana mkoa wa Lindi tunasema
shida yetu watanzania ni maendeleo na sio makelele, "aliongeza
Luponda
Pamoja na mambo Mengine
Luponda pia aliendelea kumdhihirishia Mh. Rais kuwa umoja wa vijana mkoa
wa Lindi wapo pamoja nae na wapo tayari kuungana na timu nzima
itakayoshughulikia mchakato mzima wa ununuzi wa korosho ikiwa kutakua na
nafasi ya vijana hao kushiriki katika zoezi hilo katika jitihada za
kurahisisha zoezi hilo na kuleta ufanisi.
No comments:
Post a Comment