MTAALAMU BINGWA WA NYONGA NA MAGOTI ATUA DAR.
Ashirikiana na wataalamu wazawa upasuaji Mloganzila Na Mwandishi Wetu MTAALAMU bingwa wa ubadilishaji wa nyonga na magoti kutoka hospitali kubwa nchini India ya Yashoda, Dk. Ram Mohan Reddy amewasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya kambi ya matibabu hayo kwa watanzania. Daktari huyo kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani atafanya upasuaji huo kwenye kambi ya siku tano itakayofanyika katika hospitali ya Muhimbili Mloganzila kuanzia leo Jumatatu hadi tarehe 30. Aliwasili jana usiku katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo alipokelewa na wafanyakazi wa Global Medicare ambao wameratibu kambi hiyo kwa kushirikiana na Muhimbili Mloganzila. Akizungumza kwenye mapokezi hayo, Meneja Mkuu wa Global Medicare, Daniel Lazaro, alisema wamefurahi kuona amefika salama nchini Tanzania na kwamba ujio wake utakuwa wa manufaa makubwa kwa watanzania wenye matatizo ya nyonga na magoti. “Tunajua ni mara yako ya kwanza kuja kufanyakazi na madaktari wa hapa Ta...