Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wataalam wa Maendeleo ya Jamii
kutoka Taasisi za serikali Sekta Binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali
waliojumuika katika uzinduzi wa Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela
Mkoani Arusha.
...............................
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama amewapa somo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii
nchini kuwa mfano katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuwapa mwanga
wananchi kuona mfano na kuiga na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowezesha
kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo
mwaka 2025.
Ameyasema hayo leo mkoani
Arusha alipokuwa akizindua Kongamano la Mwaka liliwakutanisha Wataalam wa
Maendeleo kutoka Wizara husika, Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa,
Halmashauri, Sekta Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Waziri Jenista amesema
kuwa katika maendeleo ya nchi yoyote Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni watu
muhimu katika kuamsha ari ya wananchi katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla katika kulueta uchechembuzi katika
utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa Serikali
imeweka mazingira wezeshi katika kuwawezesha wananchi kuchumi na kusema kuwa
katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuna jumla ya mifuko.. inayotoa
mikopo kwa waananchi ili kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara na kauanzisha
viwanda vidogo vidogo katika maeneno yao na kuwataka Wataalam wa Maendeleo ya
Jamii kuchukua mikopo hiyo na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuwa mfano kwa
jamii.
“ Nataka mkutano wa mwaka
2019 kusiwe na mabanda ya maonesho tu bali kuwe na viwanda vidogo vidogo 350
zaidi katika maeneo mnayotoka ili tuiishi kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya kufikia Uchumi wa Kati na wa Viwanda ifikapo mwaka 2025” alisisitiza
Mhe. Jenista
Aidha amempongeza Katibu
Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu kwa kusimamia Sekta ya
Maendeleo ya Jamii kwa ukaribu zaidi kwani ana uzoefu katika Baraza la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa muda aliokuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza
hilo hivyo kama atatumia uzoefu huo ataipeleka Sekta ya Maendeleo ya Jamii
mbele ili iweze kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi hasa wananchi waliopo
vijijini.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema lengo la Kongamano la
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni kuwakutanisha Wataalam hao kujadiliana mambo
mablimbali yahusuyo Taaluma hiyo ili kuja na njia na mbinu mpya za kuiwezesha
Taaluma hiyo kuendelea kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa
la Tanzania kwa ujumla.
“Mhe. Mgeni rasmi
Kongamano ni muhimu sana kwa ajili ya uhai wa Taalaum ya Maendeleo ya Jamii
ambayo ni Njini ya Maendeleo yoyote”alisisitiza Dkt. Jingu
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru Mhe. Jerry Muro amesema kuwa Maafisa na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii
ni nguzi muhimu katika maendeleo na anashangaa kwanini mpaka sasa bado tupo
nyuma katika taifa kwani kuna baadhi ya watu bado wanajivuta katika kujiletea
maendeleo katika maeneo yao.
“Mwalimu Nyerere alisema
Maendeleo yanahitaji Siasa safi tunayo, Ardhi tunayo, Watu tuano,na
Uongozi bora tuonao chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Joseph Magufuli na kwanini mpaka sasa tuko nyuma” alisisitiza Mhe. Muro.
Pia Rais wa Mpito wa Chama
cha Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Bw. Sunday Wambura amemuahidi mgeni rasmi
kuyatekeleza yale yote ambayo amewaagiza na kuhakikisha wanatumia fursa
zilizopo katika kuiwezesha jamii kuamka na kuanza kuona umuhimu wa kushiriki
katika shughuli za maendeleo yao wenyewe.
Kongamano la Wataalam wa
Maendeleo Jamii kwa mwaka 2018 lina kauli Mbiu inayosema “ Wataalam wa
Maendeleo ya Jamii ni chachu katika kufikia Uchumi wa Kati 2025” na
linafanyika kwa siku nne mfululizo Mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment