Mbunge
wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na baadhi ya wananchi wa
mtaa wa Muheza na Lumumba iliyopo kata ya maili moja katika mkutano wake
wa adhara baada ya kufanya ziara yake ya kutembelea miradi mbali mbali ya
maendeleo (PICHA NA VICTOR MASANGU)
..................................................
VICTOR
MASANGU, KIBAHA
WANANCHI WA wa mitaa miwili ya Lumumba na Muheza kata ya Pangani ,katika halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani wameanza jitihada za kujitolea kuanza ujenzi wa kivuko cha kutembea kwa miguu katika mto Mpiji kwa lengo la kuepukana na maafa ya kujeruhiwa na kuliwa na mamba kutokana na kero kubwa ya ukosefu wa kivuko cha kudumu .
Hayo
yamebainika baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kufanya
ziara yake kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo
ikiwemo kusikiliza changamoto na kero ambazo zinawakabili wananchi wake hususan
tatizo lililopo la kukosa kivuko cha kudumu na kupelekea baadhi ya wananchi
kuliwa na mamba.
Katika
kuliona hilo Koka ambaye alifika na kujionea adha hiyo ameamua kuungana
na wananchi hao na kuchangia kiasi cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya
kuendeleza ujenzi wa muda wa kukitengeneza kivuko cha watembea kwa miguu.
“Wananchi
kweli kwa sasa wanateseka sana hasa katika kipindi cha mvua na mimi tayari
nilishatoa fedha nyingine kujenga kivuko hicho lakini mafuriko yalipokuja
yalikisomba kwa hivyo nimetoa tena shilingi milioni tatu ambazo zitaweza kuanza
utekelezaji wa kujenga kivuko hiki na nawapongeza wananchi kwa ushirikiano wao
wa kujitolea kwa ahali na mali na mimi nitaendelea kuchangia zaidiili
kuondokana nah ii hali,”alisema Koka.
Pia
Koka alibainisha kuwa ,serikali ya awamu ya tano kupitia wakala wa
barabara zamijini( na vijijini TARURA )imetenga sh.mil 500
kwa ajili ya ujenzi wa kivuko hicho kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kujenga
kivuko kikubwa na cha kudumu ambacho kitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa
kuwaunganisha wananchi mbali mbali wa Wilayani Kibaha pamoja na maeneo ya
Kibwegere Jijiini Dar es Salaam .
Mwenyekiti
wa mradi huo ,Jerome Munisi alisema wameungana mitaa ya Lumumba ,Muheza na
Kibwegere (LUMUKI)kukabiliana na tatizo hilo
baada ya watu kujeruhiwa na mamba.
Alielezea,
mchango wa kaya wametoa mil 3.9,kanisa katoliki 530,000,chemchem ya uzima
750,000 jumla mil. 5.250 hivyo kwasasa mahitaji ya mafundi bado ni milioni 20
ambazo zitasaidia kujenga kivuko hicho .
Hata
hivyo ,Koka alikagua kivuko kingine cha Mkombozi kinachojengwa kwa kushirikiana
na Jeshi kwa kushirikiana na wananchi na serikali ambapo yeye alishachangia
milioni 11 na kuahidi kuendelea kuwahimiza wajenzi wa daraja ambao ni
jeshi na kwamba atawasiliana na makao makuu ya jeshi ili kuweka msukumo kitako
cha daraja kipelekwe kabla ya mvua kubwa kunyesha.
Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry koka akiangalia mradi wa ujenzi wa
shule ya msingi muheza ambao unatakuwa na vyumba vitatu vya madarasa ambapo
ukikamilika utaweza kusaidia wanafunzi kutotembea umbari mrefu kwenda kufuata
huduma ya masomo.(PICHA ANA VICTOR MASANGU)
Mmoja
wa wazee maarufu akizungumza jambo wakati wa mkutano huo wa adhara ambao
ulifanyika katika mtaa wa muheza (PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment