Posts

Showing posts from September, 2025

WANANCHI WINDE BAGAMOYO, WASHANGAZWA NA KUPANDWA MAWE MAPYA KWENYE ENEO LAO.

Image
  Wananchi wazawa wa eneo la Winde lililopo kitongoji cha Mkwajuni kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo wameshangazwa na uwepo wa mawe yanayoashiria mipaka mipya ndani ya eneo lao. Wakiongea siku ya tarehe 30 Septemba 2025 katika mkutano ulioitishwa na wananchi hao ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu eneo lao wamesema wao ndio wenye eneo hilo na tayari baadhi ya familia wamefuata taratibu za kupima eneo hilo kisheria lakini chakushangaza yanaonekana mawe katika eneo hilo. Mwenyekiti wa Wananchi hao, Muharami Seleman amesema kuwa eneo hilo ni mji wa Kale ambao una historia kubwa hivyo kuna haja ya kuuenzi kwa kuurasimisha na kuweka huduma za kijamii. Seleman amesema kuwa moja ya vitu vya kihistoria ni uwepo wa kaburi lililopo hapo tangu mwaka 1,532 la mtu mweusi, visima vya maji ambayo yanatumika hadi hivi sasa. Amesema kuwa pia eneo hilo maarufu kama namba 56 kuna mji ambao umezama baharini kwani unapakana na bahari, magofu ya kale, vyungu vya kupikia na kuna maeneo kwa ajili y...

DUA MAALUM KWA TAIFA NA RAIS SAMIA YAFANA DAR

Image
  Na Rashid Mtagaluka Tukio la Dua ya kuiombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan lililofanyika Tarehe 31 Agosti 2025 katika ukumbi wa DRIMP, Ilala Boma, ni kielelezo cha namna Watanzania wanavyotambua dhamana kubwa aliyoibeba Rais katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.  Dua hiyo iliyoongozwa na Sheikh Adam Mwinyipingu wa BAKWATA Ilala, imekusanya makundi mbalimbali ya kijamii wanawake, wanaume, vijana kwa wazee, ikiwa ni alama ya mshikimano wa kitaifa. Kinachovutia zaidi ni kwamba tukio hili limeandaliwa na mwanadada jasiri na mwandishi wa habari anayeheshimika, Fatma Jalala, kupitia taasisi yake ya Seed of Changes.  Hii ni ishara kwamba vijana, hususan wanawake, wanajitokeza mbele sio tu kama wachambuzi wa habari, bali pia kama wabunifu wa matukio yenye tija kubwa kwa taifa.  Licha ya changamoto za kiutekelezaji, Fatma hakusita kuchukua jukumu la kuandaa tukio kubwa la kuliombea taifa na kiongozi wake mkuu jambo linaloonyesha uthubutu, uzalendo na imani y...