Posts

Showing posts from February, 2020

MGUMBA ATAKA HALMASHAURI ZITENGE ARDHI KWAAJILI YA KILIMO KWA VIJANA

Image
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la vijana katika kilimo lililofanyika Njombe na kukutanisha vijana 200 toka mikoa ya Njimbe ,Iringa na Ruvuma jana. ....................................... Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga ardhi ya kutosha kwa ajili ya vijana kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi . Ametoa agizo hilo mjini Njombe wakati alipofungua kongamano la vijana wa mikoa ya Njombe,Ruvuma na Iringa kujadili fursa zilizopo katika sekta ya kilimo nchini. Mgumba amesema kumekupo na malalamiko ya vijana kukosa ardhi kutokana na halmashauri kuwa na mashamba pori mengi yasiyopimwa na kulimwa. “Halmasahauri zote zihakiki mashamba pori yote au yaliyochukuliwa mikopo na hayalimwi yapimwe na kugawiwa kwa vijana walio tayari kufanya kazi za kilimo nchini”.alisema Naibu Waziri Mgumba. Ili kufanikisha hilo Mgumba mewataka vijana kujisajili kwenye daftari...