Naibu waziri wa nishati
Subira Mgalu akisisitiza jambo katika baraza la madiwani.
......................................
......................................
Na Shushu
Joel,Chalinze.
NAIBU
waziri wa Nishati Subira Mgalu ameahidi kwenda ofisini kwa mkurugenzi wa
halmashauri ya chalinze katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa lengo la
kujionea matumizi yanayofanyika na ofisi hiyo ili kuona fedha za serikali kuu
zinavyotekelezeka matumizi yake.
Hayo
aliyasema alipokuwa katika kikao cha baraza la madiwani ambapo madiwani wengi
walikuwa wakihoji juu ya matumizi yanayofanyika bila wao kushirikishwa na
baadae wanasomewa tu kwenye vikoa kitu ambapo ni hatari katika ukaguzi na
uendeshaji wa miradi .
Aliongeza
kuwa lengo la kwenda kwenye ofisi ya mkurugenzi ni kujionea kile
kinacholalamikiwa na madiwani wenzake na kukosa majibu yenye uhakikia kutoka
kwa wataalamu wa halmashauri hiyo.
“Kumekuwepo
na matumizi ambayo si sahihi kutumika kwa kuchukua fedha za miradi hivyo mimi
kama mtaalamu wa fedha nitaenda ofisini kwa mkurugenzi kwa kuwa ni mtaalamu ili
kujionea kile wanachokifanya kupitia fedha za serikali na zile za ndani kama
kwamab vile fedha zinapokopwa kwenda sehemu zingine wanarudisha na kwenda kule
zilikopangiwa”Alisema Mgalu.
Hivyo
amemtaka mkurugenzi kuhakikisha anaandaa nyaraka ili akifika ofisini hapo aweze
kujionea kile kinachotekelezwa na ofisi yake juu ya matumizi ya fedha za
serikali kuu na zile za makusanyo ya ndani.
Aidha
waziri Mgalu amewashauri madiwani kuwa na tabia ya kumuomba mkurugenzi nyaraka
za ndani ili kujionea hali halisi ya matumizi katika halmashauri yao,kupata nyaraka ni haki ya madiwani hivyo watumie fursa
hiyo katika kujiletea maendeleo ya halmashauri yao.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya kimange Hussein Hading oka amempongeza naibu
waziri huyo wa nishati Subira Mgalu kwa kuwasaidia madiwani hao juu ya kuomba
kutambua umuhimu wa kuona nyaraka za siri juu ya matuimizi yanayoyafanya katika
ufanikishaji wa maendeleo ya halmashauri yao
ya chalinze.
Aidha
amemuomba kuendeleo kuja na kuwapatia elimu kwani madiwani walio wengi wamekuwa
hawana elimu juu ya uombaji wa nyaraka ingawa kumbe ni haki yao
ya msingi katika kutambua kile kilichofanyika katika halmashauri yao.
Naye
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Amina Kiwanuka amemkaribisha Naibu waziri huyo
wa Nishati ofisini kwake ili kujionea jinsi walivyo na matumizi bora nay ale
yanayolingana na kile kilichopangwa na madiwani pamoja na wataalamu kwa lengo
la kuhakikisha chalinze inazidi kuwa halmashauri bora hapa nchini kwa watu
mbalimbali kuendeleo kuja kujifunza katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment