Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Amina Kiwanuka,(kushoto) akizungumza jambo na Diwani wa Kata ya Talawanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu (kulia) anaesikiliza (katikati) ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa katika moja ya vikao vilivyowahi kufanyika Halmashauri ya Chalinze.
.....................................................
Na Omary Mngindo, Lugoba- Chalinze.
VIONGOZI katika Vijiji na
Kata zinazounda Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani,
wameshauliwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujiletea maendeleo, ili
waondokane na dhana kuwa watakapoanza mradi, Serikali itaongezea nguvu.
Rai hiyo imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Amina Kiwanuka, alipozungumza na
Madiwani, kwenye Baraza la kupokea taarifa za Kata, ambapo alisema suala la
maendeleo ni la wananchi wenyewe, na si kuitegemea Serikali.
Aidha Kiwanuka alisema
kuwa, inapobidi wananchi na Wadau wa maendeleo kwenye maeneo yao, washirikiane
kuendeleza miradi, kwani fedha zinapopatikana kuna mambo mengi yanayotakiwa
kufanyika katika nyanja mbalimbali.
"Nikuombe Mwenyekiti
kwa kushirikiana na viongozi wenzetu tushirikiane katika kuwapatia elimu
wananchi wetu, tutambue kwamba kazi ya kujiletea maendeleo ni yetu wenyewe,
kwakuwa tupo changamoto lazima zitukabili," alisema Kiwanuka.
Diwani wa Kata ya Miono
Juma Mpwimbwi aligusia changamoto za wingi wa wanafunzi katika shule zake,
maji, barabara ya kutoka njiapanda ya Mandera, Miono, Mkange mpaka Saadani
ambayo kipindi cha mvua hazipitiki.
"Sanjali na
changamoto hizo, pia kuna uhaba wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari
ya Kikaro, iliyoanzishwa miaka ya 58, mpaka sasa ina nyumba tano tu za walimu
naliomba Baraza liiangalie shule ile," alisema Mpwimbwi.
Mhandisi Juma Mgweno
diwani wa Kata ya Mkange aliliambia Baraza hilo kwamba kwenye eneo lake
shughuli za kimaendeleo zinafanyika, huku akisema pamoja naa shughuli za
maendeleo, uhamasishaji wa upimaji afya unafanyika kwa wananchi wake.
Zikatimu alisema kuwa
kwenye Baraza hilo zimejitokeza changamoto saba, zilizogawanyika katika sekta
za watumishi, na kwamba wamewasilisha kwa viongozi husika, maji huku akisema
kuhusu barabara watawasiliana na Wakala was Ujenzi wa Barbara Mijini na
Vijijini TARURA.
No comments:
Post a Comment