Sunday, November 11, 2018

DC. MOHAMEDI UTALY AWAONYA WAFUGAJI.

MKUU wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro Mohamed Utaly, akizungumza na wafugaji kijiji cha Sokoine kata ya Dakawa wilayani Mvomero.
.........................................................
 
Na Omary Mngindo, Mvomero

MKUU wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro Mohamed Utaly, amewataka jamii ya Wafugaji wilayani humo kuacha tabia ya kutaka kushindana na Dola, kwani hatua hiyo ni ya hatari kwa maisha yao.

Utaly ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wafugaji wanaounda umoja wao Kanda ya Mashariki, kwenye Mkutano uliofanyika Kijiji cha Sokoine, Kata ya Dakawa wilayani hapa, ambapo alisema kuwa baadhi ya wafugaji hawaiheshimu dola.

Wafugaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Morogoro Shamba Lingido, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wafugaji Taifa Joshua Lugosi na Olnjurie Marigwa Mwenyekiti wa wafugaji Mkoa wa Pwani, Utaly amewataka viongozi wa jamii hiyo kuwaonya vijana wao.

Alieleza kuwa siku moja mfugaji jamii ya Morani, alikatazwa asiingize mifugo kwenye shamba, ambapo baada ya hatua hiyo alitaka kupambana na askari Polisi aliyekuwa na siraha, tukio ambalo askari alimtaka mfugaji huyo atulie, lakini cha kusikitisha hakutii amri hiyo.

"Nampongeze askari aliyekutwa na tukuo hilo, alimzuia amsimfuate kwa kuwa alikuwa siraha mkononi, cha kusikitisha Morani huyo akiwa na mkuki mkononi, alikuwa anakwenda kwa kasi akimfuata askari lengo kutaka kumnyang'anya siraha," alisema Utaly.

Akaongeza kuwa askari baada ya kumuona Morani huyo hatii amri, akapiga risasi moja juu kama kumtisha, lakini hakutii, huku akimfuata kwa kasia, kaongeza nyingine mbili ndipo yeye na wenzake wakageuka na kuanza kukimbia.

Nae Inspekta Emmanuel Mphuru Msaidizi wa Mkuu wa Kituo aliyemwakilisha Mkuu wa Polisi wilaya (OCD) alisema kuwa kitendo cha jamii hiyo kupuuza amri za polisi no kujitakia matatizo, hivyo ni vema wakatii amri.

Akizungumzia tukio hilo, Lingindo amesema kuwa wamesikitishwa kuwepo kwa tukio hilo, na kwamba watakaa na viongozi wao kuona ni namna gani wanavyoweza kulizungumza kwa lengo laondoa hali hiyo.

Watumishi waliofutana na Mkuu wa wilaya wakifuatilia mazungumo ya mkutano huo.

Wafugaji wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly

Mwenyekiti wa Wafugaji Mkoa wa Pwani, (kulia) akifuatilia mkutano huo kwa kunukuu mambo muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa.


Pichani kutoka kushoto Mwenyekiti wa Time, Veronica Ndetiai Kindeti, letoni Leboi Mwenyekiti wa Wafugaji Kanda na Shamba kubwa Mwenyekiti wa Wafugaji Mkoa wa Morogoro, Picha zote na Omary Mngindo.

No comments:

Post a Comment