Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, akiwa mtaani kukamata watumiaji wa dawa za kulevya.
..........................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi,
amefanya operation ya kushtukiza katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dodoma na kuwa baini vijana wanaotumia madawa ya kulevya
aina ya gundi tatizo ambalo limekuwa sugu katika Jiji la Dodoma.
Katika operation hiyo Katambi amefanikiwa
kuwakamata vijana ambao wamekuwa wakitumia madawa hayo ambayo yamekuwa
yakiwaathiri vijana kwa kiasi kikubwa kwani gundi hiyo wakivuta imekuwa
ikiwalewesha.
Hata hivyo waathirika wa madawa hayo wamemuonesha
mahali ambapo wamekuwa wakinunua madawa hayo, na Mkuu wa Wilaya kuweka mtego wa
kuwanasa wauzaji hao, kwa kuwatuma watumiaji hao na kufanikiwa kumkamata
muuzaji wa duka hilo Veronica Valerian, pamoja na mmiliki wa duka hilo Hechikael Valerian.
Hata hivyo Mmiliki wa duka hilo aliwakana vijana
hao kwa kudai kuwa hawafahamu wala hajawahihi kuwauzia gundi, mara baada ya
kufikishwa katika kituo cha cha polisi kati Dodoma, wauzaji walikili kuwauzia
watoto hao, lakini wakidai mmiliki wa duka alikuwa hatambui biashara hiyo.
“Ni kweli tunawauzia gundi lakini mama hatambui
ndio maana alikataa kutambua biashara hiyo na alikuwa hatambui chochote kuhusu
swala hili na hakuona biashara hiyo.” Alisema Veronica.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Patrobas Katambi
amesema ameamua kufanya operation hiyo baada ya kuona vijana wadogo wanateketea
katika janga hilo
la uvutaji gundi ambalo limekuwa likiathiri watoto wengi hapa mjini.
“ Nimeamua kufanya operation hii kwa sababu
nimeona vijana wengi hapa mjini wanateketea katika janga hili na tusipo
chukua hatua watoto wetu wataharika zaidi, sababu janga limekuwa kubwa.”
Alisema Katambi.
Amesema na vijana wengi walioingia kwenye janga
hili si wakazi wa Dodoma, bali ni wale waliotoka nje ya Dodoma, waliokuja
kutafuta maisha lakini kutokana na umri wao kuwa mdogo wanakosa fursa hali
inayowapelekea kuingia katika janga la uvutaji wa madawa ya kulevya.
Amesema vijana hawa hununua gundi na kuiweka
kwenye vikopo na kuanza kuivuta hali inayopelekea vijana hawa kulewa, na
ukivuta gundi hii inapelekea kuhalibu mfumo wa fahamu na kupoteza uwezo wa
kufikili na kupelekea kuhalibika na kuwa vibaka mitaani.
Vilevile amezitaka jamii kulichukulia kwa uzito
swala hili kwa sababu ni kinyume na maadili yetu na kinyume na sheria za
Nchi yetu kwahiyo kila mtu anawajibu wa kuzuia vitendo hivi.
No comments:
Post a Comment