Afisa Uvuvi wilaya ya Bagamoyo Aboubakari Mposo, akizungumza na bagamoyokwanzablog.
Samaki mkubwa mwenye urefu
wa futi 36 na kimo cha futi 10 amekutwa amekufa kwenye ufukwe wa Bahari
ya Hindi katika Kijiji cha Kaole wilayani Bagamoyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Afia Uvuvi wilaya ya Bagamoyo, Aboubakari
Mposo alisema Samaki huyoanajulikana kwa jina la Chongoe ambae sio mara nyingi kuonekana kwake na kwamba bado
haijafahamika kifochake kimesababishwa na nini.
Mposo
aliwataka wananchi wanaoishi karibu na ufukwe wa Bahari
kutoa taarifa kwenye m amlaka zinazohusika mara wanapoona kiumbe
wa ajabu ili wahusika wafanye utafiti
na kubaini aina ya
kium be hicho na sababu za kifo chake.
Wananchi
katika Kijiji cha Kaole
walioshuhudia samaki huyo
wamesema wameona faraja kumuona samaki
mkubwa kama huyo am b apobaadhiya
watu hawakuwahi kufikiria kama
baharini kuna samaki
mkubwa kama huyo.
Kwa upande wao
wavuvi wazoefu katika Pwani ya
Bagamoyo wamesema kuwa Samaki
huyo aina ya Chongoe
n diy huyo anaefahamika pia kwa
jina la Nyangumi, na kuongeza kuwa samaki huyo hana shida
hata pale anapokuwa mzima na kukutana nae katika Bahari.
Kwa mujibu wa wakazi wa Kaole wamesem a Samaki huyo aligundulika katika ufukwe huo Tarehe 14 jumamosi wakati tayari akiwa am eshakufa na kwamba haifahamiki alikufa lini kwakuwa anaonekana alikufa siku kadhaa zilizopita.
Wananchi mbalimbali waliofika Kwenye ufukwe wa
Bahari kijiji cha Kaole wilayani Bagamoyo kujionea Samaki huyo mkubwa.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, kushoto
alifika kushuhudia samaki huyo, kulia ni Diwani wa kata ya Dunda, Dicksoni Makamba.
Wananchi mbalimbali walifika katika eneo hilo la
Kaole kushuhudia samaki huyo.
No comments:
Post a Comment