Posts

Showing posts from March, 2026

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 24 MACHI 2026

Image
 

SERIKALI YAHIMIZA MELI YA NEW MV MWANZA KUKUZA UCHUMI, UTALII KANDA YA ZIWA.

Image
  Serikali imetoa wito kwa wafanyabiashara, wasafirishaji na wawekezaji mbalimbali kutumia fursa ya meli mpya ya MV New Mwanza kibiashara na kiutalii ili kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa. ‎ Itakumbukwa meli hiyo imejengwa kwa zaidi ya Tsh. Bilioni 120, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa matatu na madogo, ambapo itafanya safari zake katika bandari zote zinazozunguka Ziwa Victoria ikiwemo Kisumu (Kenya), Port Bay (Uganda) na Kemondo (Bukoba). ‎ ‎Akizungumza Jumapili Machi 22, 2026 na waandishi wa habari katika bandari ya Mwanza Kusini jijini Mwanza ilipoegeshwa meli hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kutokana na uwekezaji huo wakazi wa Kanda ya Ziwa, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanapaswa kuitumia kwenye shughuli zao na kuleta tija ya uwekezaji huo mkubwa. ‎ ‎Amesema Serikali imetimiza jukumu lake la kutekeleza wajibu wa kujenga mazingira mazuri ya biashara, uwekezaji na ustawi wa jamii, hivyo mpira sasa unaha...

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA MAJI 2026

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika pamoja na Watanzania kwa ujumla kuweka kipaumbele katika utunzaji na ulinzi wa vya vyanzo vya maji ili kuweza kurithisha kizazi kijacho nchi inayofaa kuishi.   Makamu wa Rais ametoa wito huo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Maji kwa Mwaka 2026 na Siku ya Maji Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mkwawa mkoani Morogoro leo tarehe 22 Machi 2026. Amesema ni lazima kuangalia sana umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati ambao unaangalia kuvitunza na kuongeza vyanzo vya maji.   Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wizara na Taasisi zote za Umma nchini kujenga mtandao wa ushirikiano katika kuzikabili kuzitatua na kurekebisha changamoto za maji ili dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan...

MFALME WA SWEDEN AMUAGA BALOZI MATINYI

Image
  Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Mfalme wa Sweden, Carl XVI Gustaf, wakati alipokwenda kumuaga katika Jumba la Kifalme jijini Stockholm, tarehe 19 Machi, 2026 (Picha kwa hisani ya Jumba la Kifalme). ....................................................... Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden, amemuaga aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Jumba la Kifalme jijini Stockholm, jana tarehe 19 Machi, 2026.   Katika mazungumzo yao mafupi, viongozi hao walijadiliana namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika sekta za nishati, mazingira, kilimo, utalii, miundombinu, madini na teknolojia.   Mfalme Gustaf aliipongeza Tanzania kwa kuweka utulivu nchini na kubuni mipango thabiti ya kutafuta maendeleo na kukuza uchumi wake licha ya changamoto nyingi zinazoikabili dunia nzima hivi sasa.   Balozi Matinyi alimshukur...

JET YAPONGEZA JUHUDI ZA WANAWAKE KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA.

Image
  Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kinawatakia heri wanawake wote nchini na duniani katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8,2026. JET inatambua mchango mkubwa wa mwanamke katika kulinda na kuhifadhi mazingira.  Kwa muda mrefu wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika matumizi ya rasilimali asilia ndani ya familia na jamii, hivyo kuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.  Mwanamke ndiye mlezi wa familia na mara nyingi ndiye anayehusika moja kwa moja na matumizi ya nishati ya kupikia, maji, na rasilimali nyingine muhimu za mazingira. Kupitia nafasi hiyo, wanawake wameendelea kuwa kichocheo muhimu cha utunzaji wa mazingira, kwa kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali, kupunguza uharibifu wa misitu, na kuhimiza mbinu rafiki kwa mazingira katika shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi. Katika maadhimisho haya, JET pia inatoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa ...