Wednesday, April 20, 2022

RC MAKALLA: MRADI WA MWENDOKASI KILWA ROAD MBAGALA KUKAMILIKA MARCH 2023*.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewapongeza *TANROAD* kwa hatua walizochukuwa kumsimamia Mkandarasi kutoka kampuni ya *SINOHYDRO* anaetekeleza Awamu ya pili ya mradi wa *Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya mwendokasi Kilwa road.*


Akizungumza wakati wa *ziara* ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke, *RC Makalla* amefurahi kuona Ujenzi huo umefikia *Asilimia 52* ambapo amemtaka *Mkandarasi kuongeza bidii* ili kazi ikamilike kabla ya *mwezi March mwakani*  ili lengo la *Rais Samia Suluhu Hassan* kutoa huduma bora ya usafiri iweze kutimia.


Kutokana na *mwenendo Mzuri* wa Mkandarasi, *RC Makalla* ameelekeza kuwepo kwa utaratibu rafiki utakaofanya Shughuli za Ujenzi zinazoendelea *zisiathiri Shughuli za Wananchi* ikiwemo kusababisha *foleni, vumbi na hata kuzuia uzalishaji viwandani.*


Hata hivyo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD na TARURA* kumpatia *taarifa ya mgawanyo wa Majukumu* yao hususani kuweka makubaliano ya nani anapaswa kusimamia *Mifereji na Mitaro.*


Katika ziara hiyo *RC Makalla* pia ametembelea *Ujenzi wa Zahanati ya Toangoma* inayogharimu Shilingi *Milioni 250* na Zahanati ya *Kilakala* inayogharimu Shilingi *Milioni 250* ikiwa ni fedha zitokanazo na *Tozo za Simu* ambapo *amepongeza Halmashauri ya Manispaa ya Temeke* kwa kusimamia kikamilifu Miradi ya maendeleo.

Thursday, April 14, 2022

MFALME WA MOROCCO ARIDHIA KUFUNGULIWA KWA MSIKITI WA MOHAMED WA SITA ULIOJENGWA TANZANIA.

 No description available.

No description available.

Msemaji wa Mufti wa Tanzania,Katibu wa Baraza la Ulamaa Sheikh Hassan Chizenga alipozungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.

........................................

NA MUSSA KHALID

Mfalme wa Morocco Mtukufu Muhammed wa sita ameruhusu kufanyika ufunguzi mdogo wa msikiti wa Mohamed wa sita na Mpya wa Makao Makuu unaotarajiwa kuchukua waumini zaidi ya 6000 uliojengwa Kinondoni road jijini Dar es salaam.

 

Akizungumza Leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Mufti wa Tanzania,Katibu wa Baraza la Ulamaa Sheikh Hassan Chizenga amesema msikiti huo ulijengwa na Mfalme wa Morocco ikiwa ni zawadi iliyotolewa kwa waislamu wa Tanzania utafunguliwa kesho April,15 Mwaka huu.

 

Shekh Chizenga amesema kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Juhudi za viongozi wakuu wa nchi Katika awamu Mbili zilizopita Dkt Jakaya Kikwete na Hayati Dakt John Magifuli kujenga Mahusiano mazuri na Morocco jambo lililopelekea Mfalme Huyo kutembelea Tanzania na kufikishiwa ombi Hilo la ujenzi wa msikiti.

 

Aidha Shekh Chizenga amesema kuwa msikiti huo ulikuwa ufunguliwe miaka miwili iliyopita hivyo kutokana na janga la Corona lilisababisha  Mfalme wa Morocco kushindwa kufika nchini Kwa lengo la kufungua msikiti huo.

 

“Ufunguzi kamili wa msikiti huu utafanyika baadae kea kufunguliwa rasmi na Mfalme Mwenyewe Mtukufu wa sita siku za usoni pale mazingira na mipango ya tukio Hilo litakapo kamilika”amesema Shekh Chizenga.

 

Imeelezwa kuwa msikiti huo utakuwa ni miongoni mwa misikiti mikubwa Afrika Mashariki huku kwa nchi Tanzania ukiongoza kuingiza waumuni wengi zaidi ya 6000 hivyo waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuonyesha ushirikianao kwa kujitokeza kwenye ufunguzi Pamoja kuswali ibada za jamaa Kwenye msikiti huo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 14 APRIL 2022.

 No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

ASILIMIA 26 YA WATU WAZIMA WANASHINIKIZO LA JUU LA DAMU.

 No description available.

Na WAF- DOM 

MGANGA Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe amebainisha kuwa asilimia 26 ya watu wazima wenye umri wa miaka kati ya 25 hadi 64wana shinikizo la juu la damu, hali inayosababishwa na mtindo wa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula vya mafuta mengi, matumizi ya pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi.

 

Dkt. Sichalwe amebainisha hayo leo Aprili 13, 2022 wakati akifungua Mradi wa Healthy Heart Africa tukio lililofanyika katika zahanati ya Makole Jijini Dodoma.

 

“Tumefanya utafiti mwaka 2012 na kukagundua kwamba asilimia 26 ya watu wazima kati ya miaka 25 na 64 wana shinikizo la juu la damu na tatizo hili linatarajia kuongezeka kwa kiasi kikubwa endapo hatutachukua hatua.” Amesema Dkt. Sichalwe.

 

Aliendelea kusema kuwa, tafiti zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 75% ya Wagonjwa hao wenye shinikizo la juu la damu hawatumii tiba yoyote, huku akiweka wazi kuwa zaidi ya robo tatu kati yao hawajui kama wana shinikizo la juu la damu.

 

Aidha, Dkt. Sichalwe amesema kuwa, taarifa za utafiti zilizofanywa katika baadhi ya hospitali za Rufaa zimebaini kuwa, wastani wa watu 19 katika kila watu 100 wanaolazwa kwa tatizo la shinikizo la juu la damu hufariki Dunia.

 

Sambamba na hilo, ameweka wazi kuwa, hali ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa kiharusi, ambapo katika kila watu 100 wanaolazwa, watu 39 wanafariki kwa tatizo hilo la shinikizo la juu la damu, hivyo Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii ili kuongeza nguvu za kupambano dhidi ya ugonjwa huo.

 

Mbali na hayo Dkt. Sichalwe ameendelea kusisitiza juu ya kuzingatia utoaji huduma za afya kwa kufuata miongozo, huku akisisitiza weledi na umahiri wakati wa kutoa huduma ili kuepusha malalamiko yanayoweza kuzuilika kutoka kwa wananchi.

 

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amewashukuru Wadau wa PATH kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa Shinikizo la juu la damu.

 

Amesema, Ukuaji wa miji, Maendeleo ya Sayansi na teknolojia na mabadiliko ya mtindo wa maisha kwa kiasi kikubwa yanaendana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, hivyo kuwaomba Wadau kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo hasa katika miji inayoendelea kwa kasi ikiwemo Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.

 

Mpango wa Healthy Heart Africa (HHA) ni mpango wa miaka miwili unaoratibiwa na AstraZeneca katika Mkoa wa Dodoma (HF 13) na Dar es salaam (HF 22), na unajumuisha jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 35 (zahanati 25 na hospitali 10). Mradi huu unashughulikia magonjwa ya moyo na mishipa, haswa Shinikizo la damu (HTN).

No description available.

 

Wednesday, April 13, 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

 No description available.No description available.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO 13 APRIL 2022.

 No description available.

No description available.

No description available.No description available.

No description available.No description available.No description available.No description available.No description available.No description available.No description available.No description available.

No description available.No description available.

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA CDC KUDHIBITI MAGONJWA

 No description available.

Na WAF- DOM

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Tanzania (Centre of Diseases Control – CDC) Dkt. Mahesh Swaminathan katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Waziri Ummy Mwalimu ameishukuru CDC kwa kuendelea kuwa mshirika wa Karibu wa Serikali na Wizara ya Afya kwa kutoa ushirikiano na msaada katika mapambano dhidi ya Magonjwa mbalimbali ikiwemo Ugonjwa wa Virusi Vya Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria pamoja na UVIKO-19.

“CDC amekuwa mshirika wetu wa karibu katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali na katika kutekeleza afua za kuboresha ubora wa huduma za afya nchini Tanzania.” Amesema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu ametaka ushirikiano zaidi katika kuboresha na kuongeza huduma za maabara za afya ya jamii pamoja na kuboresha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ili kuwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki mapema zaidi na kuokoa maisha ya wananchi.

Waziri Ummy Mwalimu ameishukuru Serikali ya Marekani kupitia miradi na programu zinatokelezwa hapa nchini kwa kutoa msaada wa USD Milioni 22 kwa jili ya kusaidia Serikali katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 na kuhamasisha wananchi kuchanja zaidi chanjo ya UVIKO-19.

Aidha Waziri Ummy Mwalimu ameiomba CDC kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kusaidia kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika Kada za Afya kwa kutoa ajira za mikataba kwa Watanzania ili kuweza kupunguza pengo la ajira za Kada ya afya ambalo kwa sasa kuna uhaba wa asilimia 53.

Kwa upande wake Mkuregenzi Mkazi wa CDC nchini Dkt. Swaminathan ameishukuruku Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuwapa mazingira rafiki na ushirikiano zaidi katika kupambana na kdhibiti magonjwa.

“Tunaamini tupo hapa sio kwajili ya kuzuia magonjwa kuingia marekani, ugonjwa ukitokea hapa Tanzania unaathari moja kwa moja kabla ya kwenda kwingine na ndio lengo letu kuu kushirikana kwa pamoja katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali.” Amesema Dkt. Swaminathan

Dkt. Swaminathan amesema kuwa CDC imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Afya nchini katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa kutoa msaada wa dawa za kupunguza makali ya VVU, kushiriki katika tafiti mbalimbali zenye kulenga kupata tiba dhidi ya magonjwa mbalimbali pamoja na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu, Malaria pamoja na ugonjwa wa UVIKO-19 nchini.

Dkt. Swaminathan amesema kuwa milango ya CDC iko wazi muda wote kwa kutoa ushauri wa kitaalam pamoja na rasilimali katika kusaidia Serikali kuweza kutoa huduma bora za tiba kwa wananchi.

No description available.