Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
...............................................
NA TTGANYA VINCENT- RS TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeamua kuweka ulinzi katika shule
za Msingi za Manispaa ya Tabora nyakati za masomo ili kuzuia kusije kukatolekea
kwa vitendo vyovyote vya kuwazulu na kuwateka wawapo shuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia vurugu kubwa zilizotokea
leo katika Shule ya Msingi Chemuchemu baada ya kuwepo kwa hisia ya watoto
wawili kutekwa.
Alisema hadi hivi sasa hajajulikana kama kweli kuna
watoto wa Shule hiyo waliotekwa na kupandishwa katika gari aina ya Noah.
Mwanri alisema wamejaribu kufuatilia ili kujua ni watoto gani
na majina yao ya watoto waliotekwa hakuyapata na wala hakuna mzazi
aliyejitokeza kusema kuwa mtoto wake amepotea.
Alitoa wito kama kuna wazazi ambapo watoto wao wametekwa watoe
taarifa kwa Polisi au katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili hatua
ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuwatafuta.
“Kuanzia sasa nimeagiza Polisi kuongeza Doria katika maeneo ya
shule za Msingi ili kuwaondolea hofu wazazi…na kama mtu asifahamika ataonekana
maeneo ya shule achukuliwe hatua” alisema.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema vurugu hizo zilitokana na wananchi
kuwa bado na kumbukumbu ya wiki iliyopita ambapo mtoto wa miaka 6 alitekwa na
kuwawa katika eneo la Tambuka Reli.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kulifanyia uchunguzi
matukio yote na kuwataka wazazi kuwa watulivu.
No comments:
Post a Comment