Waziri wa maji Prof. Makame Mbarawa,
ametoa onyo kwa mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini kuacha tabia ya
kuwabambikizia bei za ankara za maji wateja.
Mbarawa ameyasema hayo leo jijini
Dodoma alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa watendaji wa mamlaka
za maji za mikoa na wilaya
Aidha ametoa onyo kwa wakuu wa
mamlaka hizo ambao bado wanatoza gharama za huduma kwa wateja (Services
Charges) kuacha mara moja kwani atakaye bainika mshahara wake utakatwa ili
kurejesha fedha za wateja.
Prof.Mbarawa amesema kuwa
amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja kubambikiziwa ankara za
maji na mamlaka za maji katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tusiwabambikizie wateja wetu bill za
maji kiasi ambacho hawajatumia, wananchi wamekuwa wakilalamika katika
maeneo ambayo nimekuwa nikipita kuzungumza nao nawataka watendaji wote kuacha
mara moja tabia hii”amesema Prof. Mbarawa.
Hata hivyo amezungumzia juu ya
malipo ya gharama za huduma alizitaka mamlaka zote za maji nchini kuacha kutoza
wanachi na atakae bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Mbarawa amesema kuwa mpaka sasa
anashamgaa sana kuwa Services Charge tulishaziondoa lakini bado nasikia kuna
baadhi ya mamlaka watu bado wanatozwa fedha hizi ambazo tulikubaliana kwa
pamoja kuziondoa sasa naagiza kuwa atakaye bainika hivi sasa kuwa bado
anaendelea kutoza wanachi mshahara wake utakatwa ili kufidia kiasi ambacho
wateja wamelipa
Prof. Mbarawa ameziagiza mamlaka zote
za maji nchini kuongeza udhibiti wa maeneo yanayotumika kutibu maji kwa kuweka
ulinzi ikiwemo kufungwa mifumo ya kielekitroniki.
“Kwa jambo hili naomba mfanye haraka
bila kuchelewa uwepo ulinzi wa askari pamoja na mifumo ya cctv camera ili hata
kama likiharibika lolote tunakwenda kurejea katika video na kuona nini
kilitokea nini ili muweze kutibu maji ni eneo nyeti sana leo hii ukienda nchi
kama Misri kuingia katika eneo hili lazima uwe na kibari maalum”alifafanua
Prof. Mbarawa.
Prof.Mbarawa ameitaka mamlaka ya
udhibiti wa maji na nisahti kwa kushirikiana na wizara kuona namna gani
ambavyo wanaweza kuweka utaratibu wa bei moja kwa huduma ya maji vijijini.
“Leo hii ukienda vijiji unakuta
baadhi ya maeneo ndoo ya lita 20 wananunua kwa sh. 500, wengine 200 na wengine
100 hivyo lazima tuwe na bei ambayo itafahamika kwa kila eneo ili tuweze
kuwasaidia wananchi wanyonge”amesema Mbarawa
Aidha Mbarawa ametoa onyo kwa mamlaka
ambazo zimekuwa na tabia ya kushindwa kulipa ankara za umeme pamoja na madawa
ya kutibu maji.
Prof.Mbarawa amesema kuwa katika
utawala wangu mimi kama waziri wa maji sitakubaliana na mamlaka ambazo zimekuwa
zikishindwa kulipa umeme na kutaka wizara iwalipie kutoka katika mfuko wa maji
wakati wanatoa huduma na wanalipwa
Katika kikao hicho Prof. Mbarawa
amesema wizara yake itaweka mfumo sahihi wa kuwapima wakuu wa
mamlaka za maji kwa kila baada ya miezi mitatu na atakayeshidwa ataondolewa
katika nafasi yake.
No comments:
Post a Comment