Posts

Showing posts from July, 2024

MAGAZETI YA LEO TAREHE 29JULAI 2024

Image
 

SWEETBERT NKUBA AAHIDI KULETA MABADILIKO TLS.

Image
  Na Mwandishi Wetu Mgombea wa urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Sweetbert Nkuba ameelezea namna ambavyo amejipanga kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho endapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo. Moja ya mipango yake amesema ni kuboresha miundombinu ya TLS, uimarishaji wa miundombinu ya kisheria na kiteknolojia ili kuwezesha huduma bora kwa wanachama na jamii hususani kuongeza uwekezaji katika mifumo ya kidijitali ya kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma za kisheria na kuboresha ofisi za TLS katika mikoa mbalimbali kwa vifaa vya kisasa na miundombinu bora. Jambo la pili anasema atasisitiza mafunzo endelevu kwa wanachama wa TLS ili kuhakikisha kuwa wanasheria wanakuwa na ujuzi wa kisasa na uwezo wa kushindana kimataifa ikijumuisha kuanzisha programu za mafunzo ya mara kwa mara kuhusu sheria mpya na mabadiliko ya sheria pamoja na kushirikiana na taasisi za kimataifa kwa mafunzo na kubadilishana uzoefu. La tatu anasema atahakikisha TLS inakuwa na sauti yenye nguvu...

KATIBU MKUU CCM, DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MKAPA.

Image
  CCM YATOA MILIONI 10 KUBORESHA MAJENGO YA SHULE LUPASO Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3, hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara, leo Julai 28, 2024, kuhani familia na kuzungumza na wananchi wa Lupaso. Balozi Nchimbi amesema “naomba nikiri kuwa mimi ni mwanafunzi wa hayati na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), katika kipindi chake, ndiye alinilipia ada ya kusoma chuo kikuu na alikuwa mfuatiliaji sana na alitulea vizuri, sio sisi tu, bali Watanzania wote aliwalea pia. Alikuwa mzalendo kwa nchi, alifanya mabadiliko makubwa kwa nchi yake na kwa Chama chake, lakini yote CCM chini ya Dkt Samia tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyoacha hayati Benjamin Mkapa.  Pamoja hayo nimeambiwa kero za hapa na tumezichukua. CCM inatoa shilingi milioni 10 kuanza kukarabati shule ya hapa Lupaso.” Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, ...

NANI KUUKWAA URAIS WA TLS UCHAGUZI WA IJUMAA?

Image
  Na Mwandishi Wetu KAMPENI za Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambao unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa wiki hii zinaendelea kupamba  moto ambapo wagombea wanaendelea kunadi sera wakitaka kufanya mabadiliko kwenye taasisi hiyo. Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Sweetbert Nkuba, alisema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa anataka nafasi hiyo ili akapambane na mawakili ambao hawana sifa ya kufanyakazi hiyo. TLS ni taasisi muhimu inayochangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha mfumo wa sheria na haki nchini Tanzania na kwa mwaka huu wagombea wa nafasi ya urais kwenye uchaguzi huo watakuwa sita, ambao ni Boniface Mwabukusi,  Emmanuel Muga, Ibrahim Bendera,  Paul Kaunda, Revocatus Kuuli na Sweetbert Nkuba. Nkuba alisema anauzoefu wa muda mrefu wa uongozi katika ngazi mbalimbali na kuomba achaguliwe kwenye nafasi hiyo ili afanikishe vipaumbele vitano ikiwemo kuwaunganisha wanachama wa TLS na kuhakikisha maslahi ya kiuchumi ya wanachana wa...

SHAHIDI AELEZA MUME WAKE ALIVYOPIGWA NA NATHWANI MPAKA KUZIMIA.

Image
  Na Mwandishi Wetu  SHAHIDI Kiran Lalit Ratilal (52), ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jinsi mume wake alivyopigwa na mshtakiwa Bharat Nathwan (57) hadi kupoteza fahamu kutokana na ugomvi ambao ulikuwa unaendelea wa baina yao kuhusu ujenzi uliyokuwa unaendelea katika eneo la makazi yao.   Nathwan pamoja na mke wake Sangita Bharat (54) wanaoishi Mtaa wa Mrima - Kisutu, jengo la Lohana Dar es Salaam wanatuhumiwa kwa mashtaka manne likiwemo la kujeruhi waliyoyatenda Julai 21,2023 kinyume cha sheria.   Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga, Kiran alidai kuwa anakumbuka Julai 21, 2023 alikuwa nje ya akiendelea na majukumu yake nanpia shughuli za mapambo zilikuwa zinaendelea nyumbani kwake mafundi wakiweka vigae.   Alidai kuwa, mshtakiwa Sangita alitoka ndani akaanza kupaza sauti akitaka atoe malighafi (material) yote yaliyokuwepo kwenye kibaraza hicho, wakati yote yapo upande wa Kiran Lalit Ratilal na sio upande wake.  ...

MAAFISA UANDIKISHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA KAGERA WALA KIAPO

Image
  Na Alodia Dominick,  Bukoba, Maafisa uandikishaji ngazi ya wilaya na maafisa ugavi mkoani Kagera wamekula kiapo ili kwenda kutekeleza shughuli mbalimbali za tume huru ya Taifa ya uchaguzi. Watu hao wa wameapishwa Julai 25,2024 na Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Bukoba Frorah Kaijage uapisho uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa huo. Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili mgeni rasmi Jaji mstaafu Mbarouk S Mbarouk amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kufanya kazi zao kwa ueledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo na kuwaelekeza wengine ambao hawakuwahi kushiriki zoezi kama hilo. “Wakati wa uboreshaji wa daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura, jambo hili ni muhimu na litasaidia kuleta uwazi wa zoezi zima pia mawakala watasaidia kuwepo uwazi ili kupunguza kuwepo kwa vurugu zisizo za lazima” Aidha alisema kuwa, tume imetoa vibali 157  vya asasi za kiraia kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na...