MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake
wa CCM Tanzania (UWT) Farida Mgomi amempongeza mwenyekiti wa ccm
taifa ambaye pia ni Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli kwa viteendo vyake anavyovifanya nchini kwa kuwajali watu
wanyonge ambao ndio wapiga kura wa chama tawala.
Alisema hayo alipokuwa
akizungunza ktk kikao cha kawaida kuhusu kutumia fursa zinazotolewa na
serikali kwa lengo la kuwakomboa wanawake wa Tanzania kiuchumi.
Mgomi alisema
kuwa kipindi hiki si cha kujiweka nyuma nyuma
kwani serikali ya awamu ya tano imeziagiza Halmashauri kote nchini
kuhakikisha zinawapatia kina mama mikopo isiyokuwa na riba.
"Rais Dkt John
Pombe Magufuli amekuwa kimbilio la watu wa chini hii ni kutokana na
umahiri wa ccm ktk utekelezaji wake wa ilani" Alisema Mgomi.
Aidha mwenyekiti
huyo amempomgeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kitendo
chake alichokifanya kwa wakulima wa korosho kwani ameongeza
thamani zaidi ya Chama Cha Mapinduzi kwa wakulima kuwa hakuna mkukima wa
kuteseka kipindi cha serikali ya awamu ya tano.
"Uchaguzi ujao kama
vile tunasukuma mlevi tu kwani ahadi zote zilizokuwa zimesemwa wakaati
tunajinadi tumezitekeleza kwa asilimia 90% hivyo lazima ccm
tushinde kwa kishindo " Aliongeza Mwenyekiti wa Uwt mkoa wa pwani.
Kwa upande wake Apsa
Juma amempomgeza Mwenyekiti huyo wa UWT kwa kitendo chake cha
kuwakutanisha wanawake wa mlandizi na kuwafumbua macho juu ya kutokuogopa
kukopa fedha kwa ajili ya kufanya maendeleo.
Aliongeza kuwa
kipindi hiki kimekuwa tofauti kwani kila kitu kiko wazi .
No comments:
Post a Comment