Tuesday, May 29, 2018

MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na kumpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati),
Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani),
 
Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) alipokuwa akiwashukuru Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya   kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  katika Mkutano ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Nd,Rodrik Mpogolo
Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wakinyanyua mikono juu kuashiria kuunga mkono uteuzi wa Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali wakati wa Mkutano ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akimpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akimuonesha kitu  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam,

Picha na Ikulu.


RAIS DKT. MAGUFULI AANDAA FUTARI IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na wageni mbalimbali kuchukua futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.
 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akiswalisha viongozi na waalikwa mbalimbali swala ya Magharibi kabla ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ally  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akipakua futari akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Mawaziri Wakuu Wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Sinde Warioba na waalikwa wengine wakichukua futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akiwa na Jaji Mkuu Profesa Inbrahim Juma na  Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe wakichukua futari
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) akifuatiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) na wageni wengine wakichukua futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018 
 

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakiongea baada ya kupata  futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
 Kamishna  Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akiwa na Mama Evelyn Warioba wakiwa katika futari hiyo
Waalimwa wakibadilishana mawazo baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018


TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC)

NAIBU WAZIRI SUBIRA MGALU AFAFANUA MIRADI YA UMEMEVIJIJINI INAYOENDELEA KUTEKELEZWA.

Serikali imesema itaendelea na usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kasi zaidi ili vijiji vyote vilivyoingizwa kwenye Mradi vifikiwe na umeme.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Nishati Subira Hamisi Mgalu wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo amewahakikishia wabunge kuwa Serikali kupitia wizara ya Nishati imejipanga kwa kasi mpya ya utekelezaji wa Miradi hiyo.

Naibu waziri huyo wa Nishati alisema wizara imepokea changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kusambaza umeme vijijini kwenye Miradi inayotekelezwa  kupitia Wakala wa Nishati Vijiini (REA) na kwamba tayari wizara imejipanga kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi ili kazi isipate vikwazo.

Katika kuchangia Bajeti ya wizara ya Nishati wabunge walitaka kujua vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme ni mkakati upi wa wizara kuhakikisha vijiji hivyo vinapata umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Naibu waziri Subira Mgalu alifafanua kazi zilizofanywa na zile ambazo zinaendelea kufanywa kupitia REA na kuongeza kuwa hakuna kijiji ambacho kipo kwenye mpango kitakachorukwa kwenye utekelezaji.

Alisema wizara imepokea changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa REA awamu ya kwanza ya pili na ya tatu na kwamba tayari wizara imeweka mpango mkakati wa kushughulikia kasoro zote zilizojitokeza.

Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na malalamiko ya wabunge wengi kwamba kuna baadhi ya vijiji vimerukwa, vitongoji na baadhi ya taasisi za uma hazijafikiwa na umeme tayari hayo yote yanafanyiwa kazi kwaajili ya utekelezaji

Katika kuhakikisha hayo yanafanyiwa kazi, tayari wizara imekuja na orodha ya vijiji vipya 1541 ambavyo vinahitaji kufikiwa na miradi ya REA endapo Bunge litaidhinisha.

Alisema tayari mpaka sasa vijiji 545 vimefikiwa na umeme huku vijiji 502 miundombinu inaendelea kujengwa ili navyo vifikiwe na umeme.

Aidha, alisema serikali kupitia Benki kuu imeshafungua Barua za mikopo (Leters of Credit) za bilioni 268 kwa kampuni 18 na kuongeza kuwa hali hiyo itaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi.


Naibu waziri Subira Mgalu alisema kuwa Miradi ya umeme vijijini ipo ya aina nyingi ikiwemo wa (Densification –Round I) ambapo Awamu ya Kwanza (Densification –Round I) ulianza mwezi Aprili, 2017 katika mikoa nane (8) ya Pwani, Tanga, Arusha, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Mara

Alisema hadi kufikia mwezi Mei, 2018 awamu hiyo imekamilika kwa asilimia 98. ambapo jumla ya vijiji 300 kati ya 305 vimepatiwa umeme pamoja na  kuwaunganishia umeme wateja wa awali 12,084 kati ya 53,000, ambao Gharama ya utekelezaji kwa awamu hiyo ni Shilingi bilioni 62.

Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa, Mradi wa Densification awamu ya pili utahusisha vitongoji vilivyomo katika vijiji 4,090 vilivyosalia na unakadiriwa kugharimu jumla ya Shilingi bilioni 1,938. na kwamba Awamu hiyo itaanza kutekelezwa mwezi Julai, 2018.

Naibu waziri wa Nishati aliendelea kufafanua kuwa, baada ya kubaini mahitaji ya umeme ni makubwa upo Mradi mpya unaojulikna kama Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban Rural Electrification Program) ambao utasaidia kuwafikia watu wengi maeneo hayo.

Alisema Mradi wa Peri-Urban unalenga kusambaza  umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa miji ili kuboresha huduma za kijamii na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa katika maeneo hayo.

Aidha, aliongeza kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekamilisha usanifu wa mradi wa majaribio utakaotekelezwa katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam.

Mradi huo utavinufaisha vijiji/vitongoji zaidi ya 250 na kuwaunga wateja wa awali wapatao 37,000 na kusema kuwa Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Norway kwa gharama ya Shilingi bilioni 83. na kwamba unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili,2019.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika mpango wake ni kufikisha umeme vijiji vyote 7200 ifikapo mwaka 2020 hivyo wao kama viongozi katika wizara yenye dhamana ya Nishati ni kuhakikisha wanakwenda sambamba na malengo ya Rais Dkt. Magufuli.

Wakati huohuo Naibu waziri huyo wa Nishati alisema Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imeonyesha nia ya kusaidia usambazaji wa umeme katika miji mikubwa ya Mwanza, Arusha Dodoma ambapo tayari upembuzi yakinifu unaendelea kuhusu miradi hiyo.

Aidha, Naibu waziri huyo wa Nishati ametoa wito kwa wasimamizi wa Miradi na Wakandarasi kote nchini kuwashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa, Wabunge, na Wakuu wa wilaya ili kuhakikisha Miradi hiyo inatekelezwa kwa uwazi bila ya upendeleo utakaypelekea manung'uniko kutoka kwa wananchi au wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Alisema wananchi wanatakiwa kuchangia kuunganishwa umeme kwa gharama ya 27,000 tu na si zaidi ya hiyo na kwamba ameonya wale watakaokiuka maagizo hayo.
 
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Hamisi Mgalu akitoa ufafanuzi Bungeni kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.


imeandikwa na Athumani Shomari wa bagamoyokwanza.blogspot.com. 

Saturday, May 26, 2018

KAIMU DC KIBAHA, MAJID MWANGA, ATAKA VIJANA JKT KULINDA AFYA ZAO.


Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akikagua gwaride la vijana wa kujitolea Operesheni Merelani waliopata mafunzo ya awali ya kijeshi sherehe hizo zilifanyika uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
 
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni Merelani uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
.............................................
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha Alhaj Majid Mwanga amewataka vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT kutunza afya zao ili waweze kushiriki katika shughuli za kujenga Taifa kikamilifu.

Majidi aliyasema hayo wakati wa kufunga  mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea operesheni Mererani yaliyofanyika katika kikosi cha jeshi 832 KJ-RUVU JKT.

Alisema kazi ya jeshi ni kazi inayohitai utayari, ari na afya njema hivyo askari ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo anatakiwa awe na afya iliyo imarika.

Aliongeza kuwa katika U tatu walizojifunza yaani Uadilifu, Uzalendo na Uaminifu wasisahau kuwa ni lazima kuwa na afya nzuri itakayomfanya askari kuwa mchangamfu na mwenye nguvu wa kupambana na mazingira ya aina yoyote.

Alisema kutokana na umri wa vijana hao, vipo vishawishi vingi katika jamii vinavyoweza kupelekea kufanya mambo yatakayosababisha kudhoofika kwa afya zao hivyo ni lazima wachukue tahadhari.

Alifafanua kuwa hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini hasa katika wilaya za Kibaha na Bagamoyo inatisha hivyo vijana wa JKT wanapaswa kulitambua hilo na kujua namna ya kukabiliana na hali hiyo ili kujilinda na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Katika hatua nyingine aliwataka kuishi maisha ya kiaskari kwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kama walivyoapa na kuongeza kuwa kiapo ni kifungo.

Alisema haitarajiwi askari aliyepata mafunzo na kula kiapo cha utii afanye vitendo vinavyokwenda kinyume na kiapo chake kwani yeye anapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

Kwa upande wake Mkuu JKT nchini Meja Jenarali Martini Busungu katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkuu wa utawala JKT Makao Makuu, Kanali Hawa Kodi aliwataka vijana hao waliopata mafunzo ya JKT kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na ipatikane tofauti kati yao na wale ambao hawakupata mafunzo hayo.

Alisema mafunzo hayo yatumike vizuri katika jamii na wala yasiwe kwaajili ya kuwapiga raia wema na badala yake wawe ndio walinzi wa raia na kuhakikisha wanapinga kwa namna yoyote vitendo vya kihalifu.

Aliongeza kwa kuwataka vijana hao kushirikiana na mamlaka zinazohusika ili kuwafichua waovu, wasaliti na wale wote wasioitakia mema nchi ya Tanzania.

Aidha, alisema katika kipindi hiki ambacho maadili ya kitanzania yameporomoka kwa kuiga tamaduni za watu wa kigeni, Jeshi la Kujenga Taifa lina mchango mkubwa katika kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mema ya kitanzania ili kulinda heshima ya nchi yetu katika uso wa dunia.
Alisema tamaduni za kigeni nyingi zina athari kubwa katika ustawi wa maadili ya vijana hapa nchini hivyo ni wajibu wa watanzania wote kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa katika malezzi ya vijana ili kupata wazalendo wa nchi yetu.

Awali akisoma taarifa ya vijana hao, Mkuu wa Kikosi cha jeshi cha 832 KJ-RUVU JKT, Kanali Charles Mbuge alisema vijana hao wamejifunza mambo mbalimbali ya kijeshi ikiwa ni pamoja na uvumilivu, nidhamu, na kujituma wanapopewa majukumu.

Aliongeza kuwa katika mafunzo hayo waliweza kujifunza ufugaji wa aina mbalimbali, uandaaji wa bustani za mbogamboga pamoja na kuibua vipai vya sanaa na Michezo na taaluma za aina mbalimbali..

Kanali Mbuge aliwataka vijana hao wakawe askari bora na wawe tayari kutumikia nchi yao ikiwa ni pamoja na kulinda rasilimali za nchi pindi watakapohitaika kufanya hivyo.

Aidha, alisema wakufunzi wa vijana hao wametimiza majukumu yao ya kuwajenga katika tabia njema na uzalendo na kwamba  kwa sasa wamebadilika tabia zao na kuongeza maarifa juu ya ufahamu wa mambo mbalimbali.

Wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi, vijana hao wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi wa Operesheni Meralani, walisema katika kipindi chote cha mafunzo yao waliweza kupata taaluma ya stadi za maisha na stadi za kazi kwa kujifunza kwa nadharia na vitendo kazi za mikono na ujasiliamali ikiwemo ufugaji wa kuku, Bata, Samaki, na kilimo cha bustani za mbogamboga.

Walisema elimu hiyo waliyoipata itawasaidia kujikwamua kimaisha kwa kujiongezea kipato na kuondokana na umasikini.

Jumla ya vijana 1408 wamehitimu mafunzo yao ya awali ya kijeshi katika kikosi cha jeshi 832 KJ-Ruvu JKT, ambao miongoni mwao wavulana ni 960 na wasichana 448.
 
 Kaimu Mkuu wa utawala JKT Makao Makuu, Kanali Hawa Kodi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni Merelani uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
 Mkuu wa Kikosi cha jeshi 832 KJ-RUVU JKT, Kanali Charles Mbuge akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali kwa vijana wa kujitolea Operesheni Merelani uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akipata utambulisho wa vikundi tayari kwa maonyesho mbalimbali ikiwemo gwaride la mwendo wa haraka na mwendo pole kupita mbele yake.
Picha juu ni gwaride la mwendo pole na picha chini ni gwaride la mwendo wa haraka Vijana wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi wakiongozwa na wakufunzi wao wakipita mbele ya mgeni rasmi, katika uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
Wakufunzi na maafisa wa ngazi mbalimbali wa jeshi wakishuhudia vijana wao katika kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi yaliyofanyika
uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
 
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo (kushoto) akizungumza jambo na  Mkuu wa Kikosi cha jeshi 832 KJ-RUVU JKT, Kanali Charles Mbuge (kulia).
 
Meza kuu, katikati ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, kushoto ni  Kaimu Mkuu wa utawala JKT Makao Makuu, Kanali Hawa Kodi ambae alimuwakilisha Mkuu wa JKT nchini Meja Jenarali Martini Busungu katika shughuli hiyo na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha jeshi 832 KJ-RUVU JKT, Kanali Charles Mbuge.
Wageni waalikwa, wazazi wa vijana hao, ndugu jamaa na marafiki wakishuhudia sherehe hizo za kufunga mafunzo ya awali kwa vijana wa kujitolea Operesheni Merelani uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.
  Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, akiangalia bwawa la samaki alipokuwa akikagua miradi mbalimbali ya ujasiliamali inayotekelezwa na kikosi cha jeshi cha 832 KJ- RUVU JKT. 

Picha juu na chini ni Vijana wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi katika Kikosi cha jeshi 832 KJ- RUVU JKT wakionyesha mazao wanayolima katika kikosi hicho ikiwa ni sehemu ya mafunzo waliyopatiwa.

Thursday, May 24, 2018

RC NDIKILO ATAKA WANANCHI WALINDE MISITU.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wananchi mkoani humo kuacha kuvamia maeneo hifadhi za misitu ili kuruhusu uoto wa asili kwa manufaa ya taifa.

Mhandisi Ndikilo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kukagua Hifadhi ya Msitu wa Zigua ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imevamiwa.

Akizungumza mara baada ya kujionea hali ilivyo kwa sasa katika msitu huo Mkuu huyo wa Mkoa alisema baada ya kuwaondoa wavamizi katika hifadhi za misitu za mkoa wa Pwani hali za misitu hiyo imerejea kama kawaida na kwamba sasa misitu hiyo imeanza kupendeza.

Alisema kufautia kurudi kwa hali ya kawaida katika Misitu hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema wananchi mkoani humo wanapaswa kuwa walinzi wa misitu hiyo na kwamba waache kuvamia na kufanya shughuli za kibanadamu.

Aliitaja misitu hiyo iliyopo Mkoa wa Pwani kuwa ni Msitu wa Zigua, Msitu wa kazi mzumbwi, na Msitu wa Ruvu kusini

Akizungumzia umuhimu wa Msitu wa Zigua alisema msitu huo ni mapitio ya wanyama kutoka mbuga ya wanyama Saadani kuelekea Mikumi na  Mbuga Selou

Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa, Msitu huo ndio unaweza kuhifadhi mai ya mto wami ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ya binadamu na wanyama katika hifadhi ya wami mbiki iliyopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya mashariki Caroline Malundo alisema kwa sasa Msitu huo umerejea katika hali yake ya kawaida na kwamba hata wanyama waliokuwa wametoweka wameanza kurejea.

Alisema oparesheni ya kuwaondoa wavamizi katika msitu huo iliyofanywa kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama za wilaya tatu ambazo ni Handeni, Bagamoyo na Kilindi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba mpaka sasa hakuna wavamizi ndani ya msitu huo.
 

Wednesday, May 23, 2018

WANAWAKE BAGAMOYO WAPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI.


Wanawake wa Bagamoyo wamepewa elimu ya ujasiliamali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Semina hiyo ambayo imeandaliwa na ... ililenga kuwajengea uwezo katika shughuli zao katika uzalishaji wa bidha mbalimbali.

Aidha, kinamama hao wametakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kukabiliana na ushindani wa soko.

Muwezeshai wa semina hiyo alisema ni lazima kina mama waiamini kile wanachofanya kwani kuiamini ni njia moja wapo ya kufikia malengo.

Kwa upande wao wanawake hao wajasiliamali wilayani Bagamoyo wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuzalisha bidhaa zao na kudhindwa kufikia malengo wanayojiwekea.

Walisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya ujasiliamali hali inayopelekea kinamama wengi kufanya kazi zao chini ya kiwango.

Waliongeza kwa kusema kuwa upatikanaji wa malighafi ni tatizo linalowakwamisha wengi kwakuwa malighafi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya juu au kukosekana kabisa na hatimae mjasiliamali anakata tamaa ya kuendelea na uzalishaji.

Kupitia semina hiyo kinamama hao wameiomba serikali kuwajengea mazingira mazuri wajasiliamali wanawake ili waweze kumudu kuzalisha bidhaa zao ambazo ndio msingi wa maisha yao na familia zao.

Awali akifungua semina hiyo, Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo Erica Yegela aliwataka kinamama kuwa kitu kimoja ili kufikia malengo wanayojiwekea

Alisema ni vyema wakawa kwenye vikundi ili kuweza kupata msaada ikiwemo mikopo ambayo itawasidia kuendesha shughulizao za ujasiliamli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi Bagamoyo Tedy Davis alisema tatizo linalowakwamisha wajasiliamli wananwake ni kukosa mitaji hali inayopelekea kushindwa kuzalisha bidhaa.

Alisema ipo mikakati mingi ya kuwawezesha wanawake Bagamoyo ili wajikwamue kiuchumi lakini utekelezaji wa mikakati mingi unahitaji fedha.
 
 
Washiriki wa  mafunzo hayo wakifuatilia kwa karibu.