NA
MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
SHULE
ya msingi Vikawe ,kata ya Pangani ,Mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ina upungufu
wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha ,wanafunzi 600 kusomea kwenye vyumba
vinne vinavyotumika shuleni hapo .
Aidha
wakazi wa Vikawe ,wanakabiliwa na adha ya ukosefu wa maji safi na salama hali
inayosababisha kutumia maji ya visima ambayo sio salama kwao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara wa wakazi wa Vikawe Bondeni,
Vikawe Shule na Mtaa wa Miwale, ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Kibaha
Mjini ,Silvestry Koka , mkazi Amina Seif alisikitishwa kuona baadhi ya vyumba
vya madarasa vina majani ya miba badala ya wanafunzi.
Akizungumzia
suala la ukosefu wa maji , Majawa Mtwana alisema ,hawapaswi kuwa na tatizo la
maji kwakuwa bomba limepita kwenye eneo lao .
Alisema
wangefaidika na mradi huo ulioanzia Ruvu Chini -Vikawe Shuleni hadi Miwale .
“Tunaomba
utusaidie mbunge ,hatupaswi kuishi mjini wakati tunashida ya maji ,ndoa za watu
zipo matatani kwa kukosa maji ,tunaoga maji ya visimani,tunataka ushughulikie
suala hili ili tuondokane na kero hii” alielezea.
Kaimu
afisa elimu msingi ,Ramadhani Lawoga alisema,shule ya msingi Vikawe ina jumla
ya vyumba vya madarasa saba,kati ya vyumba hivyo viwili na ofisi ya mwalimu ni
jengo la zamani ambalo limechakaa.
Hata
hivyo alisema ,nalo jengo jipya lililojengwa shuleni hapo nalo ni bovu .
Lawoga
alieleza, kutokana na hali hiyo ,vyumba vitatu kati ya saba vilivyopo ni vibovu
na hivyo vinatakiwa kujengwa upya ,ambapo wanatarajia kuanza kujenga vyumba
viwili kwa bajeti ya mwaka 2018/2019.
Akijibu
juu ya upungufu wa madarasa ,aliahidi kwenda kushauriana na mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Kibaha Jennifer Omolo ili kuangalia namna ya kukarabati
baadhi ya madarasa .
Kuhusu
changamoto ya maji ,halmashauri ya mji huo imekiri kuwepo deni la bili
walilokuwa wakidaiwa na DAWASA ya sh.milioni 4.8 ambapo imeshalipa kiasi cha
sh.milioni 3.4 na imebakia deni la milioni 1.4 .
Kutokana
na ubovu pamoja na wataalamu kutofanya kazi ya usambazaji ipasavyo ya mradi huo
,Koka alisema kinachofuata ni hatua ya uchunguzi na mradi kurudishwa chini ya
DAWASA ili kuondoa tatizo hilo .
Mbunge
huyo alilazimika kuunda kamati ya watu sita akiwemo injinia wa DAWASA Kibaha,
Injinia wa maji Halmashauri ya Mji Kibaha, Diwani wa Pangani ,katibu wa nbunge
na wananchi wawili kwa ajili ya kwenda Bagamoyo ili kufuatilia jambo hilo na
kutoa mrejesho ndani ya wiki moja .
No comments:
Post a Comment