Posts

Showing posts from September, 2022

MUFTI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI YA BAKWATA MKOA WA SINGIDA

Image
  Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (wa pili kushoto) akiongoza kuomba dua baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam  Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa katika hafla iliyofanyika Septemba 18, 2022. Kutoka kulia Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh Burhan Mlau, Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh. .......................................... Dotto Mwaibale, na Philemon Mazalla-Singida   MUFTI wa  Tanzania sheikh, Dkt. Abubakar Zubeir, Septemba 18, 2022 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) Mkoa wa Singida inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa. Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi alisema amefurahishwa na kuridhishwa na hatua iliyochukuliwa ya kuanzisha ujenzi huo kwani hayo ndiyo maendeleo yanayotaki...