Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae
pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa, akipokea Sukari kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa Kituo
cha Forodha Bandari ya Bagamoyo, Raymond Mwanisawa.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa, akizungumza mara baada ya kupokea sukari na kuikabidhi kwa wakuu wa shule za serikali.
.........................................
Serikali wilayani Bagamoyo
imekamata sukari iliyoingizwa kwa njia ya magendo na kuigawa kwa shule za
sekondari na msingi, Magereza na vituo vya kulelea watoto yatima na wale wa mazingira
magumu.
Akizungumza wakati wa
kupokea sukari na kuigawa kwa wakuu wa shule, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae
pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa alisema
wilaya ya Bagamoyo imejipanga kikamilifu kukomesha mianya yote ya kukwepa
ushuru na kwamba kila anaejaribu kutumia Bandari bubu sheria itamshughulikia.
Alisema kuwa, Serikali
inahitaji kukusanya mapato kupitia vyanzo vyake ili kuendesha mambo mbalimbli
ya kimaendeleo katika jamii kwahiyo anaekwepa kodi na ushuru huyo ni mpinga
maendeleo na serikali itamshughulikia.
Aidha, aliwataka wakuu wa
shule kuitumia sukari hiyo kwa wananfunzi kama ilivyokusudiwa na wala si
vinginevyo na kuonya kuwa, atakaetumia sukari kinyume na makusudio
atamshughulikia.
Kwa upande wao walimu
waliopokea sukari hiyo wamesema sukari hiyo itawasaidia kwenye matumizi ya
shule kwa wananfunzi.
Wameahidi kuitumia kama ilivyokusudiwa na kwamba tayari wamejipanga kuweke
udhibiti wa matumizi ili kusiwe na matumizi holela.
Awali, akizungumza wakati
wa kumkabidhi sukari hiyo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Afisa Mfawidhi wa Kituo
cha Forodha Bandari ya Bagamoyo, Raymond Mwanisawa, amesema wamemkabidhi Mkuu
wa wilaya sukari hiyo ili agawe kwenye taasisi zenye uhitaji zikiwemo shule
vituo vya kulelea watoto.
Mwanisawa alisema Mamlaka
ya Mapato nchini (TRA) kwa bidhaa kama hizo
zilizokwepa ushuru, Kamishna wa forodha na kodi ya bidhaa nchini anatoa kibali
cha kugawa bidhaa hizo ili zisije kuharibika pale zilipohifadhiwa.
Alisema sukari hiyo
imekamatwa kufuatia doria iliyofanywa na maafisa wa forodha kwa kushirikiana na
jeshi la polisi katika kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa Bagamoyo
zinalipiwa ushuru halali wa serikali.
Jumla mifuko 220 ya sukari
ambayo kila mmoja ukiwa na kilo 50 amekabidhiwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ili
kuzigawa kwa taasisi zenye uhitaji.
Sukari ikishushwa kwenye
Gari na kukabidhiwa wakuu wa shule kwaajili ya shule zao.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa, akikabidhi sukari kwa shule ya Sekondari Bagamoyo.
Picha ya juu na chini ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa mazingira magumu wanalelewa katika kituo cha MOYO MMOJA, Bagamoyo mjini.
No comments:
Post a Comment