NA HADIJA OMARY, LINDI
Jumla ya Malalamiko (74)
yanayohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake katika
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani humo,yamefikishwa katika Dawati sheria
,huku vitendo vya ubakaji vikiwa vinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa,mwaka 2017
Hayo yameelezwa na Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo, Anna Maro alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG Ofisini kwake mjini humo, kuhusiana na siku (16) kupinga vitendo
vya ukatili wa kijinsia katika manispaa hiyo
Maro alisema vitendo hivyo
vimeripotiwa kituo cha Polisi cha Lindi mjini,kupitia Dawati lake la kijinsia,
na kwamba wamefanyiwa ukatili huo,kipindi cha mwaka mmoja uliopita,kuanzia
mwezi Januari hadi Disemba 2017.
Alieleza kwamba vitendo
vya ubakaji ndio unaoongoza kwa kuwa na Idadi kubwa (39),ikifuatiwa kujeruhi na
Shambulio la mwili,iliyo na idadi (9) kila moja,Mimba za wanafunzi (7),kulawiti
(3),wakati kutelekeza familia na matumizi ya Lugha za matusi zikishika mkia kwa
kuwa na idadi ya moja kila moja.
Maro alisema katika
malalamiko hayo,yaliyofikishwa Mahakamani na kutolewa uwamuzi ni kesi tatu
zinazohusu ukatili dhidi ya kulawiti, ambapo wahusika wamepewa adhabu ya
kutumikia Gerezani kifungo cha maisha.
Pia,alisema anashangazwa
na matumizi ya Lugha ya matusi inavyoendelea kutumika na Jamii,lakini hakuna
hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika .
Hata hivyo maro ametaja
mikakati ya kupunguza tatizo hilo ni pamoja na kutumia kamati ya Mtakuwa
kufanya kazi ya kuelimisha Jamii kuanzia ngazi za Mitaa,Kata na Halmashauri
mzima ya Manispaa ya Lindi.
No comments:
Post a Comment