Mkuu
wa Wilaya ya Arumeru *Mhe Jerry Muro* ametatua Mgogoro uliodumu kwa zaidi ya
*Miaka Saba* kati ya wakulima na wafugaji wa kata ya *Malula wilayani
Arumeru* na kuwataka wakulima waendelee kulima katika mashamba ya Malula
ambayo ni ardhi ya serikali iliotengwa kwaajili ya uwekezaji wa *viwanda na
bandari kavu*
Aidha
*Dc Murro* amewataka wanasheria wanaowapotosha wakulima na *wafugaji wa vijiji
vya kata ya Malula* kwa kutumia uwepo wa migoogoro ya ardhi kwa njia ya
kujinufaisha kuacha mara moja tabia hiyo na kufuta kesi hizo mahakamani
kwani ardhi ni ya serikali na mwenye dhamana na ardhi hiyo ni *Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli*
*Dc
Muro* Amezungumza wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za
wananchi wa kata ya *MALULA* ambapo mgogoro huo umetokana na wakulima na
wafugaji kufanya maeneo ya mashamba hayo kuwa ya kwao na wengine kupeleka
mashtaka mahakamani dhidi ya wananchi walioazimwa maeneo hayo na serikali
kwaajili ya kilimo.
*Imetolewa
na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.*
No comments:
Post a Comment