BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa
kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) kwa mwaka 2018 ambapo matokeo
yanaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.76% tofauti na ufaulu wa 2017
ambao ulikuwa asilimia 72.76%.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde,
amesema katika tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9%
ikilinganishwa na 2017, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza
uko chini sana tofauti na masomo mengine (50%).
NECTA pia limewafutia matokeo watahiniwa 357 waliobainika kufanya
udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018.
“Baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua
kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019,” amesema
Msonde.
Bonyeza link hapo chini kuona matokeo ya kila shule.
Bonyeza link hapo chini kuona matokeo ya kila shule.
No comments:
Post a Comment