NA MWAMVUA MWINYI,
BAGAMOYO
MENEJA wa mkoa wa mamlaka
ya maji safi na salama (DAWASA) wilayani Bagamoyo ,mkoani Pwani, Alex
Ngw’andu ameahidi kuwa wataupokea mradi wa maji kutoka Ruvu Chini -Vikawe
Shuleni -Miwale Kibaha Mjini , ifikapo novemba 30 mwaka huu.
Ametoa ufafanuzi huo baada
ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kuunda kamati ya watu sita
wiki iliyopita, kwenda kwake kufuatilia suala hilo ili kuondoa kero ya kipindi kirefu ya
ukosefu wa maji kwa wakazi wa Vikawe.
Ngw ‘andu alisema ,kamati
hiyo imefika ofisi kwake kwa nia ya kujua kama
DAWASA itauchukua mradi wa Vikawe kutokana na halmashauri ya Mji huo
kuonekana kushindwa kuuendesha mradi ipasavyo.
Alieleza, tayari Bagamoyo
wameshaupitia mradi na wahandisi wameshapata michoro na taarifa za uendeshaji
na sasa wanajiaandaa kuufufua kwa maana kuweka umeme wa uhakika ili pampu za
kusukuma maji zifanye kazi masaa angalau16 kwa siku.
“Kufufua vizimba (DP)
vilivyopo na kuanza house connections (kusambaza majumbani) kwa wateja ifikapo
January 2019 “
“Kwa ufupi ni kwamba mradi
utapokelewa end of this month, maji na huduma iliyokuwa inatolewa awali itakuwa
restored, ikiwa ni pamoja na maboresho ya kipindi cha upatikanaji
maji”,alifafanua Ngw’andu.
Alieleza, wamekubaliana na
kamati hiyo maalumu ya mbunge Koka yenye diwani wa eneo la Pangani,
wahandisi na msaidizi wa mbunge kuwa DAWASA pia itakwenda kutembelea eneo la
huduma Vikawe jumamosi ijayo.
Kwa upande wake ,katibu wa
mbunge Method Mselewa alimshukuru meneja huyo kwa kushughulikia kero za
wananchi.
Mselewa alisema, kwa
hakika DAWASA ya sasa inakwenda kujibu kero ya ukosefu wa maji Vikawe ambayo
ilikuwa ikisababisha wakazi wa eneo hilo
kutumia maji ya visima licha ya kuwa mjini.
No comments:
Post a Comment