Posts

Showing posts from June, 2018

TAARIFA KWA UMMA JUMUIA ZA KIDINI NA VYAMA VYA KIJAMII

Image
Ofisi ya Msajili wa Jumuia za Kidini na Vyama vya Kijamii Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inazikumbusha Taasisi zote za Kidini na Vyama vya Kijamii vilivyosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kulipa Ada na Madeni waliyonayo kabla ya tarehe 30/6/2018. Sheria ya Jumuia, Sura ya 337 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 (The Societies Act) inayozisajili Jumuia za Kidini na Vyama vya Kijamii inawataka wote waliosajiliwa kulipa ada zao za kila mwaka kwani kutokulipa ada ni kukiuka masharti ya Sheria iliyowasajili. Jumuia za Kidini na Vyama vya Kijamii vinatakiwa kufika kwenye Ofisi za Msajili wa Vyama vya Kijamii na Taasisi za Kidini ili kuhakiki madeni yao hivyo kuwawezesha kulipa madeni stahiki wanayodaiwa pamoja na ada zao za mwaka huu wa fedha. Uhakiki wa madeni hayo utahusisha nyaraka mbalimbali kama vile risiti ya mwisho ya malipo, nakala ya Cheti cha Usajili na Taarifa ya Utendaji yenye saini za Viongozi wawili. Malipo yote yawasilishwe kupitia benki ya NM...

WAFICHUENI WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI.

Image
Wanafunzi wa shule za Bagamoyo wakiwa kwenye maandamano kuadhimisha wiki ya Elimu. Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli, akiongea kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo. ..................................... Wazazi na walezi wilayani Bagamoyo wametakiwa kutoa ushirikiano ili kuwafichua wale wote wanaowapa mimba wanafunzi. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu. Alisema watoto wengi hukatisha masomo kwasababu ya kupewa mimba lakini juhudi za kukomesha vitendo hivyo zinakwama kutokana na wazazi au walezi kutotoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao. Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetunga sheria kali katika kuhakikisha vitendo vya kuwapa mimba wananfunzi vinakomes...

UMITASHUMTA YAZINDULIWA CHALINZE

Image
Sehemu ya washiriki wa UMITASHUMTA wa Halmashauri ya Chalinze.   Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwangaakizungumza wakati wa uzinduzi wa UMITASHUMTA wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Omari Zikatimu, wa tatu ni Afisa Elimu msingi Zainabu Makwinya na wa mwisho ni Afisa Elimu Taaluma Miriam Kihiyo. ................................................ Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga amewataka vijana wa shule za msingi kusoma kwa bidii ili vipaji walivyonavyo wavitumie wakiwa na elimu. Majid aliyasema hayo wakatai wa uzinduzi wa mashindano ya   Uendeshai wa Michezo ya Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) uliofanyika katika viwanja vya shule ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze. Alisema michezo inaibua vipaji kwa watoto lakini ni vyema vipaji hivyo vikatumika sambamba na elimu kwani mwenye elimu hutumia vizuri kipai chake. Aidha aliwataka walimu kuwasimamia watoto mashuleni katika kuhakikisha wanapata elimu bora sambamb...

SERIKALI YA BAGAMOYO YAFANYIA KAZI MAOMBI YA WANANCHI KUHUSU MSITU WA ZIGUA.

Image
Kaimu meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (katikati) akiwaonyesha wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo mipaka ya msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.     Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga wa kwanza kushoto akizungumza na wnanchi katika kijiji cha kwa Mduma.  .......................................... Serikali wilayani Bagamoyo imepokea ombi la wnanchi katika kijiji cha Kwa Mduma kata ya Kibindu la kutaka kuongezewa eneo la makazi kutoka msitu wa Zigua. Kauli hiyo imetolew na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga wakati wa ziara ya kukagua mipaka ya Msitu wa Zigua. Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la ziara hiyo ambayo imewajumuisha kamati ya siasa wilaya ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu hitajio la wananchi wa kwa Mduma na kuona namna gani wanaweza kuwasilisha maombi ya wananchi hao ngazi za juu. Alisema kufuatia ukweli kwamba sehemu wanayodai ni muhimu kwakuwa tayari kuna zahanati ambayo inawahudumia wananchi hao, ser...

JAFO APIGA MARUFUKU MAMLUKI KUSHIRIKI UMISSETA NA UMITASHUMTA

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa mikoa yao inapeleka wachezaji wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya UMISSETA iliyoanza leo katika viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba kilichopo jijini Mwanza. Aidha amewataka waamuzi watakaochezesha mashindano hayo pamoja na yale ya UMITASHUMTA kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo hiyo kwa kuzingatia kanuni na sheria bila kuwepo upendeleo ili washindi wa michezo yote wapatikane kwa haki. Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri Jafo alieleza kuwa mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyoanza leo yatafanyika yataendelea hadi hadi Juni 15 mwaka huu. Mashindano ya UMISSETA yatafuatiwa na michezo ya UMITASHUMTA ambayo yatafanyika katika viwanja hivyo hivyo kuanzia tarehe 17 juni 2018 hadi tarehe 29 juni 2018. Waziri Jafo alieleza kuwa michezo hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi n...