Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,
...................................................
Na Omary
Mngindo, Pingo
MGOGORO wa
mpaka kati ya Kitongoji cha Pingo kinachokaliwa na jamii ya Wakulima na Kijiji
cha Chamakweza cha Wafugaji, Kata ya Pera, halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo
Pwani, unataraji kunalizika mwezi wa nane mwakani.
Mgogoro
huo uliodumu kwa miaka mingi katika eneo hilo linalopakana, umekuwa kikwazo cha
kupatikana kwa maendeleo kwa wakazi wapande hizo hali inayokwamisha shughuli
mbalimbali.
Hayo
yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alipokuwa
anazungumza na wakazi wa Kitongoji cha Pingo, siku moja kabla ya kuelekea mjini
Dodoma kwa ajili ya kikao cha Bunge kilichoanza mwanzoni mwa mwezi Novemba.
"Niwaambie
kwamba suala la mgogoro wa mpaka kati ya Pingo na Chamakweza suala lake lipo
ukingoni kumalizika, kwa sasa lipo kwa wahusika wa ardhi, niwaambie kwamba
mpaka ifikapo mwezi wa nane mwakani suala hili litabaki historia," alisema
Ridhiwani.
Aliwaambia
wakazi wa Kitongoji cha Pingo kwamba, mgogoro wa miaka mingi kati ya Kitongoji
hicho na Chamakweza utabaki histotia, huku akiwataka wakazi kuendelea na
utulivu, serikali yao inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Wakizungumza
katika mkutano huo, wakazi Mussa Matungura, na Idd Fuko walisema kuwa mgogoro
huo kwa kiasi kilibwa umechelewesha maendeleo kwa upande wa wakulima, kutokana
na mifugo kuingia kwa wingi kwenye mashamba yao.
Kwa upande
wake mzee Maarufu Rajabu Kiwamba alisema kwamba wakati wa uhai wa Mzee Kikwete
(babu yake Rudhiwani) ndie aliyewapokea wafugaji akawatengea eneo la
Chamakweza, wakati huo walikuwa wachche, kakini kadri miaka ilivyokuw inakwenda
wakawa wanaitana hatimae kuwa wengi na kuingia ndani ya Pingo.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Pingo Miraji Dibwe alisema kuwa, kuna
wawekezaji hawatambuliki na serikali wanawekeza, ambapo wanpokwenda kuzungumza
nao wanasema wamepata vibali ngazi za juu.
Kauli
iliyomkera Ridhiwani ambapo alisema kitu kama hicho hakipo, huku akisema
wananchi ndio wenye maamuzi ya kila jambo kwenye eneo lao na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment